Na Elinipa Lupembe
Uongozi wa halmashauri ya Arusha kupitia Idara za Elimu Msingi na Sekondari wamekutana na Wamiliki wa shule za binafsi za halmashauri hiyo kwenye kikao kazi cha kujadili mustakabali wa utoaji wa elimu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya serikali.
Katika kikao kazi hicho, watapata wasaa wa kujadiliana na kubadilishana uzoefu juu ya mambo yafuatayo:-
1. Usajili wa shule na usajili wa wanafunzi kwenye mfumo ili kuwa na takwimu sahihi za shule na wanafunzi.
2. Usimamizi wa Mitaala kwa kuzingatia vigezo ikiwemo, matumizi ya Vitabu vyenye Ithibati ya Taasisi ya Elimu.
3. Taratibu za uandikishwaji na uhamisho wa wanafunzi kutoka shule moja kwenda nyingine.
4. Uwepo na ubora wa Miundombinu ya shule inayokidhi vigezo vya shule.
5. Usalama na Ulinzi katika usimamizi wa mitihani ya ndani na ya Taifa.
6. Mkataba wa malipo ya ada kati ya mzazi na mmiliki wa shule na utoaji vyeti.
7. Ushirikiano baina ya Serikali na Wamiliki wa shule katika utoaji wa Taarifa za kielimu pindi zinapohitajika pamoja na kushiriki vikao vya kielimi ngazi ya Halmashauri.
8. Ulinzi na Usalama wa watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia, usalama wa vyombo vya usafiri na watoto kwenye vyombo vya usafiri.
9. Uendeshaji wa Michezo shuleni pamoja na ushiriki wa michezo ya UMITASHUMTA na UMISETA
Jumla ya wamiliki wa shule 59 za binafsi za msingi na sekondari wamekusanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha kwa lengo la kujengeana uwezo wa uendeshaji wa shule hizo.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaziInaendelea
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaziInaendelea✍✍
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KIKAO KAZI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.