Na. Elinipa Lupembe
Vijana wamekiri kutokuwa na taarifa sahihi juu ya masuala ya afya ya uzazi kwa vijana, kutokana na mila na desturi za jamii zao, zinazolazimisha wazazi kuficha taarifa za uzazi, wakiamini kuwaweka vijana wazi ni kuwaruhusu kujiingiza kwenye vitendo vya ngono.
Vijana hao wameweka wazi mtazamo huo, wakati wa mdahalo uliowahusisha wanafunzi wa shule ya sekondari Kiranyi, halmashauri ya Arusha, mdahalo ulioendeshwa na timu ya watalamu wa TCI - Tupange Pamoja, halmashauri ya Arusha.
Wanafunzi hao wamesema kuwa, wazazi wamekuwa wakali kwa vijana huku wakishindwa kiwapa watoto wao taarifa sahihi za masuala ya uzazi na mabadiliko ya makuzi yanayowakabili, na kubaki wakiwakaripia pale wanapouliza matokeo ya mabadiliko hayo, jambo ambalo linasababisha vijana wengi kupata taarifa za uzazi kwa marafiki na kujikuta wakijiingiza kwenye vitendo vya ngono na kuzimisha ndoto zao.
"Unakuta kijana unamuuliza mzazi, mimi nnatatizo flani yanayotokana na mabadiliko ya makuzi, mzazi anaanza kukugombeza umeanza umalaya, hiyo ni tabia mbaya, unaniabisha, kwenye ukoo wetu hakuna mtoto amewahi kusema hivyo, mzazi hakwambii ukweli, jambo linalotufanya tukaulize kwa marafiki ambao nao hawajui vizuri na kujikuta vijana wengi wanajiingiza kwenye ,asuala ya ngono, ulevi na uvutaji bangi, jambo ambalo mzazi angekwambia ukweli kama ninyi mnavyotwambia, matatizo mengi yasingetokea",Wamesema Vijana hao.
Aidha vijana hao wameitaka jamii na wazazi, kutoa elimu kwa vijana juu ya mambadiliko ya makuzi na uzazi ili waweze kutambua mabadiliko hayo vizuri na namna ya kukabiliana na mihemko inayoyokana na mabadiliko hayo.
Hata hivyo, katika mdahalo huo, watalamu waongoza mjadala, walipata wasaa wa kuwapa elimu ya makuzi na mabadiliko ya via vya uzazi kwa vijana, afya ya uzazi na uzazi wa mpango, na jinsi ya kukabiliana na mihemko ya ujana inayotokana na mabadiliko ya makuzi, jambo ambalo limewafanya vijana hao, kuona umuhimu wa wazazi na jamii kuwafundisha kwa uwazi, ili waweze kukabiliana na mihemko ya ujana.
Watalamu hao wamewataka vijana hao, kufika kwenye vituo vya kutoplea huduma za afya, kupata ushauri juu wa Afya ya Uzazi kupitia HUDUMA RAFIKI KWA VIJANA, huduma zinazotolewa bure kwa na kwa siri kwa vijana, huduma ambazo zitawapa uelewa mpana juu ya afya ya uzazi na namna ya kukabiliana na mihemko na vishawishi katika kipindi chote cha ujana.
Mradi wa TCI-Tupange pamoja unatekelezwa kwa ushirikiano wa halmashauri ya Arusha na shirika la JHPIEGO kwa ufadhili wa mfuko wa Bill&Melinda Gate wa nchini Marekani.
PICHA ZA MATUKIO YA MDAHALO WANAFUNZI SEKONDARI KIRANYI.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.