• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

VIJANA ARUSHA DC WAMEMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA KWA MIKOPO ISIYO NA RIBA.

Posted on: February 6th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Vijana halmashauri ya Arusha walionufaika na mikopo isiyo na riba inayotolewa na serikali, wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na mkakati wa kuwawezesha vijana kupata mitaji na kuimarisha vipato.


Vijana hao wametoa kauli hiyo, wakati wa zoezi la kupokea mikopo iliyotolewa na halmashauri hiyo ikiwa ni asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023, hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya halmashauri hiyo.


Kwa umoja wao, vijana hao wameweka wazi kuwa mpango huwa wa serikali wa kuwapa mikopo isiyo na riba imewawezesha vijana kuongeza thamani kwenye kazi wanazozifanya na kujiingiza kwenye shughuli za ujasiriamali, shughuli zinazowaongezea kipato.


Habibu Malia kijana mwenye ulemavu, aliyekopeshwa shilingi milioni 10 na kununua bajaji, amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa mpango huo wa kuwawezesha wananchi hasa vijana kujikwamua kiuchumi, mpango ambao unawainua vijana wengi hasa walioathirika na ukosefu wa ajira nchini.


Joseph Mibaroi wa kikundi cha KIDALI Youth Group cha kata ya Mwandeti, ameweka wazi kuwa awali alijishughulisha na kilimo na  ufugaji wa nyumbani, lakini baada ya kupata elimu juu ya mikopo hiyo walijuinga kikundi na kukopeshwa milioni 10 fedha ambazo zimewatoa kwenye kilimo na ufugaji wa kawaida na kuwaingiza kwenye kilimo biashara kwa kununua mifugo na kuuza.


"Tunaishukuru serikali kwa kutupa mkopo wenye masharti nafuu, hata sisi vijana wa kijijini kabisa tumeweza kukopesheka, jambo ambalo halipatikani kwenye taasisi nyingine za kifedha, mkopo umetuinua na kuingai kwenye biashara sasa". Amesema Mibaroi


Naye Paulo Paskali amesema  kuwa uchache wa vikundi vya vijana kujiingiza kwenye mikopo ni uoga na kushindwa kujiamini huku wengine wakidhani vikundi ni vya kinamaa, na kuiomba serikali kuendelea kuwajengewa uwezo wa kujiamini na namna bora ya kukopa, kwa kufanya hivyo vijana wanaweza kufanya mapinduzi ya kiuchumi kwenye jamii.


Aidha ameipongeza serikali, licha ya kutoa mikopo, watalamu wake wanafanya kazi kubwa sana ya kuelimisha na kuwaunganisha vijana ili wakidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo, jambo ambalo linathamani na matokeo makubwa kwa vijana wa kitanzania, vijana ambao baadhi yao, ndoto zao zilikuwa zimeanza kufifia kwa kupoteza matumaini.


 Hata hivyo vijana walikopeshwa wamewasihi vijana wote nchini kujitokeza kutumia fursa hiyo adhimu, ili waweze kujipatia mitaji ya kukuza pato la kijana mmoja mmoja, familia na jamii kwa ujumla wake.


Serikali kupitia halmashauri zote nchini inatoa mikopo isiyo na riba kwa kutoa 10 % ya mapato ya ndani kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kiuchumi.


ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"

#KaziInaendelea✍







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.