Na. Elinipa Lupembe.
Wanufaika wa mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, mradi unaotekelezwa Serikali kupitia Mfuko wa Maendelo ya Jamii - TASAF III awamu ya pili, wameanza kunufaika kiuchumi kupitia vikundi vya kuweka na kuwekeza, vikundi vilivyoviunda na walengwa hao, halmashauri ya Arusha.
Walengwa hao wa kijiji cha Oltulelei kata ya Ilboru, wameweza kuinua vipato vya familia zao kwa kujipatia mitaji ya kuanzisha miradi midogo midogo, kupitia programu ya vikundi vya TASAF vya kuweka, kuwekeza na kukopa.Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye maeneo ya biashara zao, wana kaya hao wamethibitisha kuwa, licha ya kupokea fedha za ruzuku ya mwezi, lakini pia walijengewa uwezo wa kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa kupitia fedha za ruzuku wanazopokea.
Janeth John mlengwa na mwenyekiti wa kikundi cha UPENDO -TASAF anayemiliki genge la kuuza mbogamboaga kwa sasa, amesema kuwa watalamu waliwajengea uwezo wa kuanzisha vikundi vya kuwekeza pesa kutokana na ruzuku wanayoipa kutoka TASAF,na bada ya kuanzisha kikundi kimewawezesha kupata mitaji na kuongeza kuwa kila mwanakukundi ameshaanzisha biashara yake sasa Kikundi chetu kina wana wanachama 10, tulianza tukiwa na hofu sana, lakini kikundi kimetuwezesha kupata mitaji ya kuanzisha biashara, biashara ambazo zimepunguza ugumu wa maisha, biashara zimewawezesha wanakikundi hao kuwekeza, kukopa na kurejesha kwa wakati, na kuongeza kuwa, walipoanza kikundi wengi wao hawakuwa na biashara, na kwa sasa wanachama wote wana biashara, biashara ambazo zimewawezesha kujimudu kimaisha kwa kila mmoja mwanakikundi.
"Hapo mwanzo hatukuamini kama jambo hili kama litawezekana, kutoka na kiasi cha oesa tunachopokea, lakini tumeweza kugonga hisa kila wiki, tuna mfuko wa jamii ambao tunasaidiana kutatua changamoto za kijamii kama msiba na ugonjwa, lakini zaidi tumeweza kukopeshana na kupata mitaji, inayotuwezehsa kuendelea kuweka akiba, kukopa na kupata marejesho, huku faida ya biashara ikituwezesha kuhudumia famialia zetu " amesisitiza Janeth.
Rabisante Mwanga, mwanakikundi cha UPENDO na mama wa watoto watatu, amebainisha kuwa, kupitia kikundi chao cha UPENDO TASAF, ameweza kupata mtaji wa shilingi 150,000 wa kuuza mitumba, mradi ambao unampatia kipato cha kumudu maisha yake na familia yake huku akiwa na matarajio ya kukuza mtaji na kuanza kununua mitumba kwa jumla maarufu kama 'belo'.
Dina Yoram, mlengwa anayemiliki genge na sehemu ya kuchoma samaki na mihogo, amefafanua kuwa, Kikundi chao kimewawezesha kuongeza kipato cha familia yake, na kumfanya kumudu mahitaji ya muhimu kwa familia yake na kuwataka wanawake waaibweteke badala yake kutumia futsa hizo za vikundi kuanzisha biashara ili kupambana na hali ya umaaikini.
Hata hivyo Dina Emson, amewaka wazi kuwa kabla ya kuanza kupokea pesa za TASAF alikuwa na ujuzi wa kusuka, akisuka wateja wake eneo lisilo rasmi, baada ya kujiunga na kikundi cha TASAF amefanikiwa kufungua saloon, eneo ambalo limemuwezesha kupata wateja zaidi, mtaji ambao unamudu kulipa kodi ya pango pamoja na kuhudumia familia yake.
"Nilikuwa na ujuzi wa kusuka nawafuata wateja nyumbani, jambo ambalo lilinigharimu nauli ya kwenda na kurudi, kwa sasa wateja wangu wananifuata hapa hapa saloon kwangu, kadri siku zinavyokwenda natarajia kuweka vifaa vyote vya saloon na saloon yangu iwe kubwa zaidi"amesistiza Upendo.
Mpango wa Kunusuru kaya masikini, wenye lengo la kukuza pato la familia, umekuwa na programu ya vikundi vya kuweka na kuwekeza kwa walengwa walio kwenye mpango ili kukuza uchumi wa kaya
program ambayo imeanza kuzaa matunda kwa baadhi ya Kaya hizo.
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI
JIANDAE KUHESABIWA 23. 8.2022
Janeth John, mlengwa na mwenyekiti wa kikundi cha UPENDO - TASAF akiwa kwenye genge lake la mbogamboga, biahsara ambayo mtaji wake ameupata kutokana na kikundi cha kuweka na kuwekeza.
Rabisante Mwanga, mlengwa na mwanakikundi cha UPENDO - TASAF akitembeza biasha yake ya kuuza nguo za mitumba, mtaji ambao ameupata kutokana na kikundi cha kuweka na kuwekeza.
Genge la Dina Emson, mlengwa na mwanakikundi cha UPENDO - TASAF, genge ambalo mtaji wake ameupata kutokana na kikundi cha kuweka na kuwekeza.
Dina Emson, mlengwa na mwanakikundi cha UPENDO - TASAF akimsuka mteja ndani ya saloon yake, biashara ambayo mtaji wake ameupata kutokana na kikundi cha kuweka na kuwekeza
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.