Na. Elinipa Lupembe.
Mradi wa maji wa Ngaramtoni na moja ya miradi wa maji ya vijiji kumi umekamilika na unategemea kutumia teknolojia mpya ya 'eWaterpay' ya kulipia maji kabla ya kutumia.
Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, wakati akifungua mafunzo ya siku nne yanayohusisha wafanyakazi na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Ngaramtoni (NGAUWSA), kwenye Ukumbi wa mikutano wa Golden Rose.
Mkurugenzi Mahera amesema kuwa mradio huo wenye thamani ya shilingi milioni mia 7.9, unaotegemewa kukabidhiwa mapema wiki ijayo na tayari vituo 21 vya kuchotea maji vimeanza kutoa maji kwa majaribio na vyote vitafungwa mfumo wa 'eWaterpay' wa kulipia maji kabla ya kutmia.
Hata hivyo Dkt. Mahera amefafanua kuwa, mfumo huo unafanyika kwa majaribio, baada ya kuona mafanikio ya mfumo huo, waliyoyapa wananchi wa mkoa wa jirani wa Manyara kwenye halmashauri ya Babati.
Mkurugenzi Mahera, amethibitisha kuwa, mfumo huo unauwezo wa kudhibiti mapato pamoja na kudhibiti upotevu wa rasilimali maji, unaokwenda sambamba na utunzaji wa rasilimali maji hasa kwa kukizingatia kuna changamoto ya upatikanaji wa maji,kwenye vyanzo vya maji.
"Tunatarajia teknolojia ya 'eWaterpay' kuboresha utaratibu mzima wa utoaji huduma ya maji pamoja na upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi" amesema Mkurugenzi.
Aidha Dkt. Mahera amewataka watumishi na wajumbe wa Bodi ya Maji - NGAUWSA kutumia mafunzo hayo, kuongeza kiasi cha upatikanaji wa huduma za maji ndani ya maeneo yote ya Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni.
Naye Mratibu wa shirika la eWater, Deogratius Nyusso, amethibitisha kuwa, teknolojia ya 'eWaterpay' inarahisisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa watumiaji wa maji na kwa watoa huduma ya maji pia, na inauwezo wa kutatua changamoto za miundo mbinu ya maji kwa haraka zaidi,kwa kuwa mfumo unaruhusu kuona changamoto hizo ukiwa ofisini bila kufika eneo husika.
"Teknolojia hii inamrahisishia mtumia maji kudhibiti matumizi yake binafsi ya maji, kwa kulipia maji aliyoyatumia, pamoja na kuirahisishia NGAUWSA kudhibiti ukusanyaji wa mapato, kufahamu endapo kuna uharibifu wa miundombinu ya bomba, bila kufika eneo la tukio na kuweza kutengeneza kwa wakati" amethibitisha Nyusso.
Nyusso ameongeza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watumishi hao kwenye maeneo ya ukusanyaji mapato kwa uwazi na uhakika, kupitia teknolojia rahisi ya kutumia simu sambamba na utatuzi wa changamoto za mifumo ya maji.
Naye Meneja wa NGAUWSA, Clayson Kimaro, ameonyesha namna matumizi ya teknolojia hiyo, yatakavyorahisiha upatikanaji wa huduma za maji kwa wananchi pamoja na uwezekano wa kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma hiyo katika eneo linalohudumiwa na NGAUWSA.
Hata hivyo, teknolojia hiyo ya 'eWaterpay' itatumika zaidi kwenye mradi wa maji wa maji vijiji vitano, unaofadhiliwa Idara ya maendeleo ya nchini Uingereza 'DFID' na kutekelezwa na shirika la WaterAid Tanzania, unaotegemea kukamilika mwishonj mwa mwezi Septemba 2018 na unategemea kuhudumia watu elfu hamsini.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.