Na. Elinipa Lupembe.
Kundi la Wadau wa maji wa shirika la WaterAid, kutoka nchini Uingereza 'Water Supporters', wametembelea mradi mkubwa wa maji wa Vijiji Vitano, unaotekelezwa na shirika hilo ndani ya halmashauri ya Arusha, na kujionea shughuli za utekelezaji wa mradi huo zinavyoendelea.
Wadau hao, wamefanya ziara hiyo kwa lengo la Kuangalia jinsi, utekelezaji wa mradi huo unavyoweza kuhudumia wananchi kwa wakati wote na kwa kipindi cha muda kirefu.
Akizungumza na wadau hao, wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, amesema kuwa, mradi huo ni mkubwa, kuwahi kutekelezwa katika halmashauri yake, ukiwa na teknolojia ya malipo ya kabla, teknolojia inayoaminika kuwezesha upatikanaji wa maji wa uhakika muda wote, pamoja na kuhudumia wananchi wengi kwa miaka ishirini ijayo.
Ameongeza kuwa, utekelezaji wa mradi huo, umetoa fursa ya ushirikishwaji wa wananchi wa eneo nufaika la mradi, kwa kuwajulisha hatua kwa hatua katika utekelezaji wa mradi huo, jambo linalowafanya wananchi kufahamu vizuri mradi huo.
Hata hivyo, wadau hao, wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo wa maji huku wakipongeza zaidi, ushirikishwaji wa wananchi katika hatua zote za mradi, pamoja na teknolojia ya malipo ya kabla, itakayowezesha uhakika wa jamii kupata maji kwa miaka ishirini ijayo.
Mradi wa maji wa vijiji vitano, unatekelezwa katika halmashauri ya Arusha, kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza kwa gharama ya shilingi bilioni 8.4, unategemea kukamilika mwaka huu wa 2019 na kuhudumia watu elfu hamsini na kufikia asilimia 70 ya wananchi wa halmshauri hiyo kupata maji safi na salama
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.