Na Elinipa Lupembe
ASAS za kiraia zinazojihusisha na masuala ya elimu, halmashauri ya Arusha, wamekutana na kujadili mstakabali wa elimu na kupanga mkakati wa pamoja namna bora ya kuboresha na kuendeleza sekta ya elimu bila kuathiri sheria na sera ya elimu nchini.
Wadau hao, wamekutana katika kikao kazi cha siku moja kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya msingi Green Acres, kikiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kati ya idara za elimu za halmashauri na ASAS za Kiraia ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuanda mkakati wa kuendeleza sekta ya elimu.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi hicho, Katibu Tawala wilaya ya Arumeru, Mwl. James Mchembe, amebainisha kuwa serikali imetoa fursa kwa ASAS za kiraia kushiriki katika kutekeleza mpango mkakati katika sekta ya elimu, hii ni kutokana na ukubwa wa mahitaji usioendana na uwezo wa kirasilimali.
Amesema kuwa ASAS za kiraia ni kiungo cha msingi sana katika kutekeleza vipaumbele vya serikali vya kutoa huduma za jamii kisekta na kusisitiza kuwa, licha ya kuwa serikali inatekeleza majukumu yake lakini mafanikio ya elimu nchini yanapewa nguvu na ASAS za kiraia.
"Serikali inathamini kazi zenu mnazozifanya kwa niaba ya serikali, natumaini matokeo ya kikao kazi hiki, yanaenda kutoa suluhishi na dira ua utatuzi wa changamoto za elimu, kwa lengo la kumkomboa mtoto wa Arusha DC kifkra kupitia elimu".Amefafanua Mwl. Mchembe.
Maafisa Elimu Msingi na Sekondari, walielezea dira, maono, malengo na mwelekeo wa elimu katika halmashari hiyo na kubainisha changamoto zinazokwamisha kufikia malengo ikiwemo upungufu wa miundo mbinu, utoro unaosababishwa na ukosefu wa chakula kwa shule za kutwa, watoto kuchelewa kuandikishwa shule kutokana na umbali wa shule pamoja na uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa elimu ya awali.
Hata hivyo wadau hao, wameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo kwa kuona umuhimu wa kukaa pamoja na kupanga mipango ya pamoja yenye kunia mamoja katika kutekeleza mikakafti ya elimu na kufikia malengo ya serikali.
Kikao kazi ni kizuri, kimetupa nafasi ya kufahamiana kila ASAS na shughuli zake, lakini zaidi kuifahamu mikakati ya idara ya elimu na kuona namna ya sisi kama ASAS kujipanga kujumuika katika kutekeleza mikakati, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira bora na kupambana na adui ujinga, kwa manufaa ya watoto na Taifa kwa ujumla". Amesema Ang'weni Lang'o wa Shirika la A is for Africa.
Hata hivyo, wadau hao wa elimu, wameahidi kushirikiana na halmashauri, kuhamasisha wazazi na jamii kutambua majukumu yao kwa watoto wao ikiwemo suala la kuchangia vhakula cha watoto wanaosoma shule za kutwa.
Mratibu wa miradi, shirika la ACE Africa, Bugesi Matayo amebainisha kuwa, wazazi wamekuwa na mawazo potofu juu ya sera ya elimu bure, na kujiweka pembani na kuacha kuwahudumia watoto wao husuani kuwahudumia chakula cha mchana kwa wanafunzi wa kutwa.
Aidha Wadau hao wa Elimu wamekubaliana kwa kukaa pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Arusha, kupanga mipango ya pamoja kwa mwkaa ujao wa masomo unaoanza 2023, ikiwa na lengo la kuboresha sekta ya elimu kwa kutatua changamoto zanazowakabili wanafunzi shuleni.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Selemani Msumi amezisisitiza ASAS za Kiraia kutokuchoka kuisaidia jamii hususani watoto ambao wanaoandaliwa kulitumikia taifa hili huku wakiwa na ndoto za kutimiza katika maisha yao kupitia elimu,zaidi ni utekeleazaji wa ilani ya CCM wa kuimarisha mashirika ya Umma ili yaweze kuendelea kutoa, michango katika maendeleo ya Taifa.
"Tunafahamu elimu ni msingi wa maisha, Wadau mnalo jukumu la kushirikiana na serikali kuhakikisha watoto wanapata elimu bora, katika mazingira bora bila vizuizi vinavyoweza kuzilika, tukiunga kwa pamoja, tukania mamoja katika kusukuma gurudumu hili la elimu kwa mtoto wa kitanzania, tutafikia malengo ya serikali ya kuoambana na adui ujinga, umasikini na maradhi". Amesisitiza Msumi.
ARUSHA DC
KaziIendelee✍✍✍
Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl. James Mchembe (katikati) akizungumza na wawakilishi wa ASAS za kiraia zinazofanya shughuli za Elimu Halmashauri ya Arusha wakati akifungua kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa idara za Elimu na Wadau wa Elimu kwenye ukumbi wa shule ya msingi Green Acres.
Mkuu wa idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Arusha Mwl. Menard Lupenza akizungumza na wawakilishi wa ASAS za kiraia zinazofanya shughuli za Elimu Halmashauri ya Arusha wakati kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa idara za Elimu na Wadau wa Elimu kwenye ukumbi wa shule ya msingi Green Acres.
Mkuu wa idara ya Elimu Msingi Halmashauri ya Arusha Mwl. Salvatory Alute akizungumza na wawakilishi wa ASAS za kiraia zinazofanya shughuli za Elimu Halmashauri ya Arusha wakati kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa idara za Elimu na Wadau wa Elimu kwenye ukumbi wa shule ya msingi Green Acres.
Baadhi ya wawakilishi wa ASAS za kiraia zinazofanya shughuli za Elimu Halmashauri ya Arusha wakati kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa idara za Elimu na Wadau wa Elimu kwenye ukumbi wa shule ya msingi Green Acres.
Baadhi ya wawakilishi wa ASAS za kiraia zinazofanya shughuli za Elimu Halmashauri ya Arusha wakati kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa idara za Elimu na Wadau wa Elimu kwenye ukumbi wa shule ya msingi Green Acres
Picha ya pamoja na mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl. James Mchembe, wawakilishi wa ASAS za kiraia na wataalamu wa Halmashauri ya Arusha, wakati kikao kazi kwenye ukumbi wa shule ya msingi Green Acres.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.