Na. Elinipa Lupembe
Wafadhili wa Jaykat Shah Foundation na Made with Hope wa nchini Uingereza, kwa kushirikiana na shirika la Ndoto in Action la nchini, wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa kutatua changamoto za jamii hususan katika sekta ya elimu.
Wafadhili hao Jaykany Shah na Alexander Margolin kwa pamoja, wamefikia uamuzi huo, mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi wanayoifadhili inayotekelezwa na shirika la Ndoto in Action, ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya shule za msingi Mshikamano na Marurani, kata ya Nduruma halmashauri ya Arusha.
Aidha katika ziara hiyo, wafadhili hao wameshiriki hafla ya makabidhiano ya vyumba 11 vya madarasa vilivyofanyiwa ukarabati mkubwa, madawadi 65, miundombinu ya kuvuna maji, kwa gharama ya shilingi milioni 75, mradi uliotekelezwa na shirika la Ndoto in Action katika shule ya msingi Marurani na kuaahidi kuendelea kufadhili miradi katika shule nyingine za msingi kutoka na uhitaji mkubwa waliuona.
"Lengo letu ni kusaidia jamii ya watanzania, hasa watoto kusoma katika mazingira rafiki, tumeridhishwa na miradi iliyofanyika na kuona inasaidia watoto tuliowakusudia, tunaahidi kuendela kutoa support zaidi, ili watoto wakitanzania wapate elimu katika mazingira bora" amesisitiza Jaykhan
Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo, mkurugenzi wa shirika la Ndoto in Action, Hussein Hassan, amesema kuwa shirika linashukuru kwa ushirikiano wanaoupata kutoka kwa serikali na shirika linaununga mkono juhudi na kasi ya maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya sita, kwa kuboresha sekta ya elimu na kuweka mazingira rafiki shuleni.
"Shirika linatambua changamoto ya miundombinu inayozibili shule nyingi nchini ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, uchakavu wa majengo, upungufu wa madawati, miundombinu ya vyoo pamoja na maji, vifaa vya kisasa vya kufundishia licha ya juhudi kubwa inayofanywa na serikali, kuboresha miundombinu ya shule, sisi kama shirika tuko bega kwa bega na serikali" ameweka wazi Hussein
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, kadhalika amewashukuru wafadhili hao, kwa kukarabati miundombinu ya shule ya msingi Marurani, na kuwataka walimu na wanafunzi kuendelea kuitunza miundombinu hiyo ili iweze kuwasidia kama yalivyokuwa malengo ya wafadhili hao na serikali pia.
"Serikali inatambua na kuthamini michango ya wadau wa maendeleo kwa kuwa wanafanya kwa niaba ya serikali, walimu, wanafunzi na wazazi tunalo deni la kurejesha fadhila kwa wafadhili hawa, inatubidi kuhimiza watoto wetu kusoma kwa bidii, pamoja na kutunza miundombinu hii, walimu hakikisheni wanafunzi wanatumia miundombinu yote kwa utaratibu unaofaa" amesisitiza Mkurugenzi Msumi.
Aidha wanafunzi wa shule ya msingi Marurani, licha ya kuwashukuru wafadhili waliotekeleza mradi huo, wamethibitisha mradi huo utawaongezea ari ya kusoma kwa bidii, kwenye mazingira rafiki na kupandisha kiwango cha taaluma shuleni hapo, huku wakiahidi kufaulu katika masomo yao.
Hata hivyo mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Marurani, amethibitisha kupandisha kiwango cha taaluma shuleni hapo, na kuongeza kuwa kwa miaka mitatu mfululizo sasa shule inafanya vizuri kwa kushika nafasi za juu kitaaluma kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa na hata ngazi ya Taifa.
Ikumbukwe kuwa awali, shirika la Ndoto in Action, lilifanya ukarabati wa vyumba 4 vya madarasa, ujenzi wa choo cha wasichana chenye sehemu ya kujisitiri wasichana wakati wa hedhi, na kuongeza maadarasa 11 na kukamilisha ukarabati wa jumla ya madarasa 15, katika shule ya msingi Marurani yenye jumla ya wanafunzi 424.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
#sensayawatunamakazi
#jiandaekuhesabiwa 23.08.2022
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, wa kwanza Kulia, akishirikiana na wafadhili kukata utepe, ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya vyumba 11 vya madarasa, vilivyokarabatiwa na wadau hao, shule ya msingi Marurani.
Mkurugenzi wa shirika la Ndoto in Action, Hussein Hassan, akifungua mlango wa chumba cha darasa, mara baada ya makabidhiano ya vyumba 11 vya madarasa shule ya msingi Marurani.
Mwenyekiti wa Bodi ya shirika la Made with Hope ya nchini Uingereza, Alexander Margolin akizungumza na hadhara ya jumuia ya shule ya msingi Marurani, wakati wa makabidhiano ya vyumba 11 vya madarasa vilivyokarabatiwa kwa ufadhili wa shirika hilo.
Mkurugenzi Mtendaji halmasahuri ya Arusha, Seleman Msumi, akimkabidhi cheti cha shukurani, Mkurugezni wa shirika la Jaykat Shah Foundation, Jaykhan Sha wakati walipokabidhi vyumba 11 vya madarasa walivyokarabati kupitia shirikanla Ndoto in Action, shule ya Msingi Marurani
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.