Wajumbe wa Balaza la Madiwani Halmashauri ya Arusha waipongeza Serikali inayoongonzwa na Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri ikiwemo miradi ya Afya,Elimu,Miundombinu,Maji,pamoja na umeme.
Pamajo na pongezi hizo Balaza hilo la Madiwani Halmashauri ya Arusha,wametoa rai kwa ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Arusha kuendelea kushirikiana na watalaamu kutoka Taasisi nyingine za umma kama vile AUWSA,RUWASA,TARURA,TANESCO Ili kufanikisha utatuzi wa changamoto ndani ya Kata wanazoziongoza.
Balaza la hilo Madiwani Halmashauri ya Arusha limekaa kikao chake cha robo ya kwanza ya mwaka kwaajili ya utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa miradi kwa Kata zote 27 kabla ya kukaa kwa Balaza kuu la Madiwani linalotarajiwa kufanyika tarehe 5/11/2024.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.