Wajumbe wa Kamati ya Fedha Halmashauri ya Wilaya Arusha wakiongozwa M/Kiti Dkt.Ojung'u Salekwa (mwenye shati jeupe) wakitembelea na kukagua ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Loovirukunyi iliyopo Kata ya Kisongo. Majengo ya shule hiyo yamegharimu shilingi 584,000,000 za Kitanzania chini ya mradi wa SEQUIP.
Kamati hiyo imeridhishwa na shughuli za ujenzi huo na kuwapongeza Wataalam wa Halmashauri kwa usimamizi madhubuti wa fedha za Serikali na kwa sasa shule hiyo imeshaanza kupokea wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa mwaka 2025.
Ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari Loovirukunyi imekuwa mkombozi kwa watoto waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufuata masomo hususan wa Kata za Kisongo na Matevez na kupunguza msongamano kwa shule ya Sekondari Einiot iliyopo Kata ya Kisongo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.