Na Mwandishi wetu.
Kamati ya Mpango Mkakati wa Kupambana na Kutokomeza Ukatili halmashauri ya Arusha (MTAKUWWA), imetakiwa kubuni mbinu mpya za kukabiliana na ukatili wa kijinsia ili kupunguza ongezeko la vitendo vya kikatili wa kijinsia vinavyotendeka katika jamii.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha ambaye ni mwenyekiti wa kamati MTAKUWA halmashauri hiyo, Seleman Msumi, katika mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa wanachama wa kamati ya MTAKUWWA yaliyofanyika katika ukumbi wa chama cha walimu Tanzania.
Mkurugenzi Msumi amefafanua kuwa suala la ukatili wa kijinsia ni mtambuka hivyo Serikali yenyewe haiwezi kumaliza tatizo hilo bila kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali ili kuifikia jamii kwa urahisi zaidi kwa kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia yanaleta madhara makubwa katika kizazi kijacho.“Ni imani yangu kuwa asasi zisizo za kiserikali kwa kushirikiana na Serikali zikifanya kazi kwa kushirikiana zitaleta mabadiliko chanya na kuisadia jamii kuepukana na ukatili wa kijinsia”. Amesisitiza Msumi.
Naye mwezeshaji wa mfunzo hayo, Philbert Mashingia ameweka wazi kuwa, mabadiliko yanaanza na mtu mmoja mmoja hivyo ni jukumu la kila mzazi kujitathimini na kama yeye mwenyewe ndiye chanzo cha kusababisha ukatili wa kijinsia badala ya kuitupia lawama jamii inayomzunguka.
Aidha wa Pamoja na wadau walioshiriki katika mafunzo hayo wamebainisha baadhi ya sababu zinazopelekea ongezeko la ukatili wa kijinsia, ni pamoja na mila na desturi zilizopitwa na wakati kama vile ukeketaji na ndoa za utotoni na kuwataka wazazi kuonyesha ushirikiano ili kutokomeza vitendo hivyo vya kikatili.
“Kuna changamoto kama vile suala la rushwa lakini tutajitahidi baada ya mafunzo haya kuendelea kutoa elimu kwa mtu mmoja mmoja ili jamii ipate uelewa juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia kwani wahanga wakubwa ni watoto na wanawake”. Amesema Joseph Piniel, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.
Hata hivyo, Afisa Maendelo ya jamii halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa amesema kuwa, kwa sasa jamii inapata taarifa kuhusu ukatili wa kijinsia na wako tayari kuonyesha ushirikiano kwa kuibua zaidi matukio ambayo yalikuwa yanafumbiwa macho hapo awali. Mafunzo ya wajumbe wa MTAKUWA yanatolea na shirika la Shalom Center na kushirikiana na shirika la UZIKWASA, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wajumbe hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kuifikia jamii na kutokomeza ukatili wa kijinsia.
ARUSHA DC
KaziIendekee ✍✍
JIANDAE KUHESABIWA
PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya MTAKUWWA Seleman Msumi, akitoa mchango wake wakati wa mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa wanachama wa kamati hiyo kuhusu namna ya kukabiliana na Ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi akiwa na wanakamati wengine kwenye majadiliano katika makundi
Mwezeshaji wa mafunzo ya Ukatili wa kijinsia, Philbert Mashingia akitoa mafunzo kwa wanakamati wa MTAKUWWA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.