Na. Elinipa Lupembe.
Wakulima wa zao la Pareto halmashauri ya Arusha, wameanza kunufaika na kilimo cha zao hilo, baada ya kupatfa mafunzo na usimamizi wa karibu kutoka kwa watalamu wa kilimo, huku kukiwa na soko la uhakika wa zao hilo mara baada ya mavuno.
Wrvakulima hao wamethibitisha hayo, wakati wa hafla maalumu ya siku ya mafunzo kwa wakulima wa Pareto, maarufu kama 'Field Day', iliyowakutanisha wakulima wa Pareto, halmashauri ya Arusha, hafla iliyofanyika kwenye ofisi ya kijiji cha Engalaoni kata ya Mwandeti.
Mitaro Ninjake, mkulima wa Pareto kijiji cha Engalaoni amethibitisha kuwa, kilimo cha Pareto kimeanza kuwaletea mafanikio katika kuinua pato la familia, kuliko mazao mengine ambayo walilima hapo awali, na kusisitiza kuwa pareto ni zao la uhakika ambalo kwa kipindi kifupi, wameweza kuvuna na kuuza zao hilo.
Ninjake mesema kuwa, wao wanavutiwa na kilimo cha Pareto, kutokana na uhakika wa soko la kuuza , zao hilo pindi wanapovuna tofauti na mazao mengine ambayo huwalazimu kuuza kwa bei ndogo kipindi cha mavuno.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, wakati wa siku hiyo maalumu kwa wakulima wa Pareto, Katibu Tawala, Wilaya ya Arumeru, mwalimu James Mchembe, amewapongeza wakulima hao kwa kuamua kujikita kwenye kilimo cha Pareto, zao ambalo linamanufaa kwao kiuchumi lakini pia, na linaendana na Tanzania ya viwanda kwa kuwa ni malighafi inayohitajika kiwandani kwa ajili ya kutengenezwa viwatilifu vya kuulia wadudu waharibifu.
Amewataka wakulima hao, kuongeza bidii katika kilimo cha zao la Pareto kwa kuwa ni zao linalohitajika sana kwenye soko la ndani na nje, na kuwataka kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujiongezea kipato sambamba na kujiinua kiuchumi.
Kwa upande mwingine KatibuTawala huyo, amewapongeza zaidi wakulima hao wa Pareto kwa kuacha kujihusisha na kilimo cha zao haramu la bangi na kuingia kwenye zao halali la biashara ambalo ni zao la Pareto na kuwasisitiza, kutumia mafunzo wanayopatiwa na watalamu wa kilimo ili kulima kilimo bora na kupata zao bila la pareto ambalo linauzwa kwa bei nzuri na kuweza kuwaongezea kipato na uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
"Ninawapongeza kwa kuacha kilimo haramu la bangi na kujikita kwenye kilimo halali zao la Pareto, niwasisitize kulima zao ambalo ni halali, acheni kulima bangi katika maeneo yenu, zao la Pareto linafaida kubwa na soko lake lipo wazi" amesema Katibu Tawala huyo.
Naye Mratibu wa zao la Pareto Tanzania, Maiko Bishubo amesema kuwa, lengo la siku hiyo muhimu kwa wakulima wa pareto, ni kuwaelimisha na kuwahamasisha wakulima wa Pareto mbinu bora za kutunza mashamba ya Pareto, namna ya kudumisha ubora wa zao hilo pamoja na kukabiliana na changamoto za kilimo hicho, ili kuongeza tija kwenye uzalishaji.
Amesema kuwa licha ya Kampuni ya TPC kutoa mafunzo kwa wakulima wa Pareto ,kampuni hiyo hununua Pareto iliyo bora kwa bei ya shilingi 2,300 kwa kilo, bei ambayo inawanufaisha wakukima wa zao hilo.
Diwani wa kata ya Mwandet, amesema kuwa kihistoria, za3o la pareto lilikuwepo miaka mingi na badaye wakulima kuacha kulima kuftokana na kukosa soko, kwa sasa wakukimaqw wameanza tena kujikita kwenye kilimo cha zao la Pareto, zao ambalo linahitajika ndani na nje ya nchi, soko lake n5i kubwa na liko wazi na kuongeza kuwa bado jitihada za kuhamasisha wakulima kulima zao hilo zinaendelea.
Afisa Kilimo Mazao, halmashauri ya Arusha, Rose Masawe, amesema kuwa mpaka sasa jumla ya wakulima 200 wanajuhusisha na kilimo cha Pareto kutoka kata za Oldonyosamb, Olkokola na Mwandeti huku uzalishaji ukiongezeka mwakt4a hadi mwaka.
Kwa kipindi cha miaka mitatu sasa, Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na Kampuni ya Pareto Tanzania- 'PCT' , wanawahamasisha wakulima kujikita kwenye kilimo cha Paretco na kutoa mafunzo ya kitalamu juu r4ya kilimo cha zao hilo huku kukiwa na sokso la uhakika la zao hilo la Pareto.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.