Na Elinipa Lupembe
Wasimamizi wa shule ikiwemo wakuu wa shule za sekondari na Maafisa Elimu kata wametakiwa kusimamia vigezo 12 vya usimamizi wa taaluma shuleni, ili kufikia lengo la serikali la kuketa matokeo chanya na makubwa kwenye elimu ya sekondari nchini.
Rai hiyo imetolewa na kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Arusha, Elizabeth Ngobei, lengo likiwa kufiki vigezo ambavyo vimetolewa na serikali kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuhakikisha kila kigezo kinafanyiwa kazi na kupimwa utekelezaji wake kila miezi mitatu ya robo ya mwaka.
Aidha amewataka wasimamizi hao wa elimu kuendelea kusimamia utoaji wa elimu kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni ili kujiweka kwenye nafazi nzuri katika utendaji kazi.
"Mkataba huu unavyo vigezo 12 vya kuzingatia kuanzia ngazi ya Taifa na kila ngazi ina majukumu yake lakini watendaji wakubwa ni ninyi walimu na wanafunzi, fanyeni tahmini ya utendaji kama ilivyoelekezwa zaidi hakikisheni mnaiwezesha halmashauri kufikia malengo hayo ya serikali". Amesisitiza Kaim Mkurugenzi.
Naye Mkuu wa Idara ya Elimu sekondari, halmashauri ya Arusha Mwl. Menard Lupenza, amevitaja vigezo hivyo 12 kuwa, ni pamoja na kusimamia utoaji wa taaluma kwa kuboresha ufundishaji na ujifunzaji, kuhakikisha wanafunzi wote waliopangiwa kidato cha kwanza wanaripoti shuleni.
Kudhibiti utoro na kupunguza mdondoko wa wanafunzi, kusimamia utoaji wa chakula shuleni hasa kwa shule za kutwa, kuboresha matokeo ya mitihani ya ndani na ile ya Taifa kwa kuondoa alama F na kufanya tahmini ya matokeo pamoja na kuainisha changamoto, kuhakikisha wanafunzi wanajifunza na kuijua lugha ya kiingereza.
Ameongeza kuwa wakuu wa shule wanawajibu wa kuhakikisha masomo yote yanafundishwa kwa ufasaha huku walimu mahiri wakifundisha kidato cha kwanza, pamoja na kuwalinda watoto dhidi ya vitendo viovu vya ukatili na udhalilishaji.
Aidha ameahidi kuwasimamia watendaji wote walio chini yake kwa kuhakikisha kila mmoja anatekeleza wajibu wake pamoja na kuhakikisha walimu wanapata stahiki zao pamoja na mafunzo kazini huku akisisitiza kuwachukulia hatua wale watakao kwenda kinyume au kukwamisha utekelzaji wa vigezo vilivyoainishwa kwa namna yoyote.
Hata hivyo wasimamizi hao wa elimu ngazi ya shule na kata, wamebainisha kuwa vigezo vilivyoanishwa vikifanyiwa kazi vina tija kwa kuwa vinaondoa kasumba ya utendaji kazi wa mazoea na kuwawezesha kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na kwa uwanda mkubwa.
Mkuu wa shule Kiranyi, Mwl. amesema kuwa vigezo vilivyoainishwa una tija kubwa ukiwa umegusa maslahi ya mwalimu na wanafunzi na kuongeza kuwa walimu kwa sasa wanaenda kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia vigezo vya upimaji, vigezo ambavyo vitamlazimu mwalimu kuwajibika ili kufikia malengo.
Awali wakuu wa shule za sekondari halmashauri ya Arusha pamoja na Maafisa Elimu wa kata zote wamesaini mkataba wa kazi wa kusimamia Elimu, zoezi lililoambatana na kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Taifa ya kidato cha nne mwaka 2022.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaziInaendelea✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.