• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WALENGWA TASAF WATAKIWA KUTIMIZA MASHARTI YA RUZUKU YA FEDHA WANAZOPOKEA

Posted on: September 21st, 2022

 Na Elinipa Lupembe

Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF awamu ya IV, wametakiwa kutimiza masharti ya msingi ya ruzuku ya fedha wanazozipokea ili kuimarisha sifa za kuwa kwenye mpango.

Akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji ruzuku ya fefha kwa mwezi wa 7/8, 2022, Mratibu wa TASAF halmashauri ya Arusha, Grace Makema, amesema kuwa, TASAF inatoa fedha hizo kwa walengwa zikiwa na masharti ya kutimiza, ili mlengwa aendelee kuwa na sifa za kupokea ruzuku hiyo.

Amewataka walengwa hao kuzingatia masharti hayo, ikiwa ni pamoja na masharti ya afya kwa kaya zenye watoto wa kuanzia miaka 0-5, kwa kuhakikisha watoto hao, wanahudhuria kliniki kwa kipindi chote, pamoja na kupata chanjo zote stahiki kwa miaka hiyo mitano.

Ameongeza kuwa, kaya pia zinatakiwa kuzingatia masharti ya elimu, kwa kaya zenye watoto wa miaka 6-18, kuhakikisha wanakwenda shule na kuhudhuria masomo ya kwa siku zote bila kukosa huku wakiwapatia watoto hao mahitaji muhimu ya shule.

"TASAF imeandaa utaratibu wa kufanya Warsha za Jamii, ili kutoa mafunzo kwa walegwa kila wakati wa zoezi la kugawa ruzuku, hivyo tunasisitiza kila mlengwa kuhudhuria warsha za jamii, ili kuendelea kupata ufahamu zaidi wa huduma zinazotolewa na mpango, haki, wajibu na umuhimu wa kutimiza masharti ya ruzuku" . Amefafanua Mratibu Grace.

Hata hivyo walengwa wa kijiji cha Laroi, wamepongeza, serikali kupitia TASAF kwa kuziwezesha kaya zao kiuchumi, huku wakiendelea kupewa elimu ya matumizi ya fedha na kutambua haki na wajibu wao kama wanufaika wa mpango huo,

Mwenyekiti wa kijiji cha Laroi, Mhe. Remingi Joseph, amebainisha kuwa uwepo wa program mbalimbali za mafunzo kwa walengwa unasaidia walengwa na jamii kupata uelewa wa pamoja juu ya miradi ya TASAF na ruzuku za fedha wanazopokea walengwa.

"Mradi wa TASAF licha ya kuwainua kiuchumim lakini pia umewafanya wananchi kuchangamsha akili na kubadilika kifikra kwa kuwa wanajumuika na wenzao kwenye vikundi na miradi lakini zaidi wanapata mafunzo yanayowawezesha kubadilika na kukua kifikra" Ameweka wazi mhe. Remigi

Awali katika dirisha la mwezi wa 7/8, jumla ya shilingi milioni 617.1, zimetolewa kwa kaya 12,288 katika vijiji 88 vya halmashauri ya Arusha, huku kaya hizo zikipokea fedha kwa njia ya mitandao ya simu, benki, mawala na fedha tasmu.


ARUSHA DC,

TUPO KAZINI.

Mwenyekiti wa kijiji cha Laroi, Mhe. Remigi Joseph, akiwahudumia walengwa wa mpango wa Kunusuru kaya masikini waliofika kupokea ruzuku ya malipo ya mwezi 7/0 2022, kwenye ofisi ya kijiji hicho.


Afisa Mtendaji wa  kijiji cha Laroi, Saning'o Moiyo, (aliyeshikamkaratasi) akisoma majina ya wanakaya mpango wa Kunusuru kaya masikini waliofika kupokea ruzuku ya malipo ya mwezi 7/0 2022, kwenye ofisi ya kijiji hicho.


Mwenyekiti wa kijiji cha Lemanda, Mhe. Moses Kalombo, akiwahudumia walengwa wa mpango wa Kunusuru kaya masikini waliofika kupokea ruzuku ya malipo ya mwezi 7/0 2022, kwenye ofisi ya kijiji hicho.

Wanakaya wa kijiji cha Laroi, wakisubiri taratibu za malipo ya ruzuku ya malipo ya mwezi 7/0 2022, kwenye ofisi ya kijiji hicho.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.