Na Elinipa Lupembe
Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF, wametakiwa kutimiza masharti ya ruzuku ya fedha wanazozipokea ili kuimaarisha sifa za kuendelea kuwa kwenye mpango pamoja na kufikia malengo ya serikali..
Akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa ruzuku ya dirisha la 13/14, Mratibu wa TASAF halmashauri ya Arusha, Grace Makema, amesema kuwa, TASAF inatoa fedha hizo kwa walengwa walio kwenye mpango, zikiwa na masharti ya kutimiza, ili mlengwa aendelee kuwa na sifa za kupokea ruzuku hiyo pamoja na kufikia malengo ya kuondoa umaskini nchini
Amewataka walengwa hao kuzingatia masharti hayo, ikiwa ni pamoja na masharti ya afya kwa kaya zenye watoto wa kuanzia miaka 0-5, kwa kuhakikisha watoto hao, wanahudhuria kliniki kwa kipindi chote, pamoja na kupata chanjo zote stahiki kwa miaka hiyo mitano.
Ameongeza kuwa, kaya pia zinatakiwa kuzingatia masharti ya elimu, kwa kaya zenye watoto wa miaka 6-18, kuhakikisha wanakwenda shule na kuhudhuria masomo ya kwa siku zote bila kukosa huku wakiwapatia watoto hao mahitaji muhimu ya shule.
"TASAF imeandaa utaratibu wa kufanya Warsha za Jamii, ili kutoa mafunzo kwa walegwa kila wakati wa zoezi la kugawa ruzuku, hivyo tunasisitiza kila mlengwa kuhudhuria warsha za jamii, ili kuendelea kupata ufahamu zaidi wa huduma zinazotolewa na mpango, haki, wajibu na umuhimu wa kutimiza masharti ya ruzuku" Amefafanua Mratibu Grace.
Hata hivyo walengwa wa kijiji cha Nduruma wameipongeza, serikali kupitia TASAF kwa kuziwezesha kaya zao kiuchumi, huku wakiendelea kupewa elimu ya matumizi ya fedha na kutambua haki na wajibu wao kama wanufaika wa mpango huo,
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Dkt. Ojung'u Salekwa, amewakumbusha wanufaika hao kutumia fedha hizo za ruzuku kwa malengo, huku wakihakikisha kiasi kidogo kinawekwa kama mbegu ya kuanzisha miradi midogo ambayo itawezesha fedha hiyo kuendelea kujizalisha jambo ambalo litasaidia kuinua uchumi na pato la familia.
"Ni ukweli pesa haijawahi kutosha, ukishindwa kutunza kidogo unachokipata hata ukipewa kikubwa hutaweza, kinamama serikali inawaamini na kuwapa dhamana ya kuwa wasimamizi wa kaya zenu, jiwekeeni akiba kupitia vikundi vyenu"
PICHA ZA MATUKIO WATALAMU WAKITOA WARSHA ZA JAMII KWA WANUFAIKA WA TASAF WAKATI WA MALIPO
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.