• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WALIMU ARUSHA DC WATAKIWA KUZINGATIA KUJISOMEA KUPITIA PROGRAMU YA MEWAKA

Posted on: May 24th, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Walimu halmashauri ya Arusha, wametakiwa kutumia fursa inayotolewa na serikali ya kupitianprogramu ya  Mafunzo Endelevu kwa Walimu Kazini (MEWAKA), mafunzo yenye lengo la kuboresha utalamu kitaaluma kwa walimu, ili kuwa mahiri katika mbinu za ufundishaji zinazoendana na wakati.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, wakati akifungua semina ya Mafunzo ya Walimu Kazini, iliyojumuisha walimu wakuu wa shule za msingi pamoja na Maafisa Elimu wa kata zote za halamshauri hiyo, semina iliyofanyika kwenye Ukumbi wa shule ya Msingi Green Acress.

Mkurugenzi Msumi, amewataka walimu hao, kutumia fursa hiyo, inayotolewa na serikali kuhakikisha wanapanga muda wa kujifunza zaidi kupitia miongozo na utaalam uliotolewa kwenye moduli za MEWAKA, mafunzo ambayo yatawawezesha kupata maarifa mapya na mbinu shirikishi za ufundishaji, pamoja na kufanya tathmini kwa wanafunzi.

"Serikali inatambua na inathamini kazi kubwa inayofanywa na walimu, na kuona umuhimu wa kuandaa mkakati wa MEWAKA, utakowewezesha kapata mafunzo kazini, hivyo nitoe wito kwenu viongozi wa shule, kuratibu na kusimamia mpango huo katika maeneo yenu ya kazi, ili kufikia malengo ya serikali ya kuinua kiwango cha taaluma shuleni" amesisitiza Mkurugenzi Msumi.

Naye Afisa Elimu Msingi halmashauri ya Arusha, Salvatory Alute, amefafanua kuwa, lengo la semina hiyo kwa viongozi hao wa elimu ngazi ya kata na shule ni kuwajengea uwezo wa kuratibu na kusimamia programu ya MEWAKA katika maeneo yao ya kazi, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kuwa wathibiti ubora wa ndani ya shule, kufuatilia utekelezaji wa MEWAKA na kufanya tathmini, kuwawezesha wadau wa elimu katika kupanga gharama za uendeshaji wa mafunzo na upatikanaji wa rasilimali pamoja na usimamizi wa rasilimali hizo.

Hata hivyo Afisa Elimu huyo, amebainisha kuwa mfumo wa MEWAKA umeondoa changamoto nyingi zilizokuwepo za  mifumo iliyotumika hapo awali ya mafunzo kwa walimu, hivyo programu ya MEWAKA ni mfumo rasmi ambao umeandaliwa na Serikali kutekeleza mtaala wa elimu msingi, unaozingatia umahiri wa mbinu za kufundishia na kujifunzia, kufanya tathmini kwa wanafunzi,  pamoja na kuendeleza  mafunzo hayo kwa kuhawilisha taaluma kwa walimu wote.

"MEWAKA imeandaliwa na Taasisi ya Elimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, kwa kuzingatia mitaala ya elimu inaozingatia umahiri, ndani yake kuna moduli mbalimbali zitakazowawezesha walimu kujinoa kitaaluma na kuwa mahiri katika ufundishaji pamoja na kujifunza namna ya kuendeleza mafunzo hayo kwa walimu wote ili kuwa na umahiri unaoendana na wakati" amefafanua Afisa Elimu Alute.

Aidha  walimu hao wameweka wazi kuwa, MEWAKA imekuja wakati muafaka, kutokana na kasi ya maendeleo ya kisayansi, yanayotokana na mabadiliko ya teknolojia, mabadiliko yanayomlazimu mwalimu kujisomea sana ili kupata maarifa mapya, huku wakithibitisha kuwa, program  ya MEWAKA, inawapa walimu fursa endelevu ua kujinoa kitaaluma kwa kusoma na kubadilishana uzoefu wa kazi.

Mwalimu Mkuu, shule ya Msingi Ngaramtoni, mwalimu Makanjo Twaty, amesema kuwa program ya MEWAKA ni muhimu kwa walimu, na watahakikishia kutumiammuda wa ziada kujifunza miongo yote iliyoainishwa bila kuathiri ratiba za masomo kwa wanafunzi, huku akisistiza kuwa MEWAKA itawafanya walimu kufundisha kwa kuendana na wakati, hasa kwa walimu waliosoma miaka mingi iliyopita.

"Kwa mwalimu kama mimi, niliyeanza kazi miaka ya 80, nisiposoma ninapitwa na wakati kabisa, lakini kupitia MEWAKA kila mwlaimu atalazimika kujisomea na kupata maarifa mapya, yatakayotuwezesha kwenda na wakati, munaotokana na mabadiliko ya teknolojia" ameweka wazi Mwalimu Twaty.

Awali matarajio ya  programu ya Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini, ni kuwawezesha walimu kufanyakazi kwa weledi, kusaidiana, kushirikiana, kutoa maoni kiuzoefu na kistadi katika ufunzaji na ufundishaji, kuinua matokeo ya ujifunzaji kwa wanafunzi pamoja ma kuwezesha umiliki kwa kile ambacho walimu wanajifunza kwa kuwa wanapata ya kupanga na kuamua nini cha kujifunza na kwa wakati gani.

SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

"JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022"✍✍


Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akifungua semina ya Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA), semina iliyojumuisha walimu wakuu wote wa shule za Msingi na Maafisa Elimu Kata, iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Msingi Green Acres.

Afisa Elimu Msingi, halmashauri ya Arusha, Salvatory Alute, akiwasilisha mada wakati wa semina ya Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA), semina iliyojumuisha walimu wakuu wote wa shule za Msingi na Maafisa Elimu Kata, iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Msingi Green Acres.


Walimu wakuu wa shule za msingi na Maafisa Elimu kata, halmashauri ya Arusha, wakiwa kwenye semina ya Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA), semina iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Msingi Green Acres.

Baadhi ya walimu wakuu na Maafisa Elimu kata, wakiwa kwenye majadiliano ya vikundi wakati wa semina ya MEWAKA, iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya msingi Green Acress.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.