• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Walimu shule nane Arusha DC wanufaika na mpango wa mafunzo kazini kupitia mradi wa QUEETS

Posted on: February 25th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Jumla ya shule nane za Msingi, halmashauri ya Arusha zimenufaika na mpango wa mafunzo kazini, unaotelewa na shirika la Inter- cooperation ( HELVETAS) la nchini Uswis kupitia Mradi wake wa Uboreshaji Elimu kwa mpango wa Mwalimu Mahiri (QUEETS), mradi unaotoa mafunzo kwa walimu waliopo kazini kwa masomo ya msingi, Hisabati, Kiingereza na Sayansi.

Walimu kutoka shule hizo nane,  za Naurei, Sekei, Bangata, Laroi, Ng'ires, Nambere, Oldadai, na Olgilai, wameweza kupatiwa mafunzo ya mbinu mpya na rahisi  za ufundishaji, pamoja na utengenezaji wa zana za kufundishia na kujifunzia, zinazotokana na mazingira wanayoishi.

Wakizungumza wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau wa elimu wa  mradi huo, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, makao makuu ya CWT mkoa wa Arusha, walimu hao wamethibitisha kupata utalamu wa mbinu bora za kufundishia na kujifunzia, mbinu ambazo hazimchoshi mwalimu na mwanafunzi, huku zikiwajengea wanafunzi uwezo wa kuelewa na kumbukumbu ya muda mrefu wa kitu walichojifunza.

Katika kikao hicho, Mwalimu Athman Makale wa shule ya msingi Sekei kata ya Kiutu, amesema kuwa, mpango huo wa mafunzo umewafanya walimu kupenda kazi yao na kumudu kufundisha masomo hayo matatu kwa umahiri zaidi, jambo ambalo hapo awali walimu wengi walikwepa kujifundisha masomo hayo kwa kuyaona kuwa ni magumu.

Ameongeza kuwa licha ya mpango huo kuwawezesha kufanya kazi yao ya ufundishaji kwa umahiri mkubwa, mafunzo hayo yamewawezesha kujiamini na kuwa na uhusiano mzuri kati ya walimu na wanafunzi, kutokana na kutumia zaidi njia shirikishi inayowafanya wanafunzi kupenda masomo.

"Mpango huu wa mafunzo umetuwezesha walimu kufundisha kwa kushirikiana kama timu, umetufanya kujiamini kwa kile tunachofundisha, pamoja na kuwa na uhusiano wa karibu na wanafunzi, kwa kuwa muda mwingi tunawashirikisha wanafunzi kujifunza kwa vitendo zaidi" amesema mwalimu Makale

Denis Elisha, mwanafunzi wa shule ya Msingi Naurei, amesema kuwa, kwa sasa walimu wao wanawafundisha kwa vitendo zaidi na kutumia zana za kufundishia, huku wakiwapa nafasi wanafunzi hao kufanya mazoezi ya jambo wanalojifunza wakati wa somo linapoendelea pamoja na kuwafundisha lugha ya kiingereza kwa kiingereza tofauti na hapo awali.

Ameongeza kuwa zamani walimu wao walikuwa wakiingia darasani na kuwafundisha kwa kuongea mwanzo mpaka  mwisho na kuondoka bila kujali wameelewa au hawajaelewa, jambo ambalo lilikuwa linawapa wakati mgumu wanafunzi hao kuelewa walichojifunza, lakini sasa walimu hao huwashirikisha kuanzia utengenezaji wa zana za kujifunzia, wakati wa  tendo zima la kujifunza wawapo darasani na kuhakikisha wameelewa.

"Walimu wetu zamani walikuwa hawako karibu na sisi, tulikuwa tunawaogopa, unakuta mwalimu anaingia darasani anafundisha kwa kuongea mwenyewe mwanzo mpaka mwisho wa kipindi, anamaliza na kuondoka bila kujali tumeelewa au la, lakini sasa tunawapenda walimu wetu, tunashirikiana hadi kutengeneza zana za kujifunzia, tuko huru na walimu" amesema Denis.

Afisa Elimu halmashauri ya Arusha, Mwalimu Hossein Mgewa amesema kuwa mradi wa QUEETS , umesaidia kuwajengea walimu uwezo wa kufundisha kwa kutumia zana rahisi na njia shirikishi jambo ambalo limesaidia kupanda kwa taaluma kwa shule za msingi, na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hasa wale wanaofanya mitihani ya taifa ya darasa la nne na la saba.

Naye Meneja wa Mradi wa shirika la HELVETAS, Donathian Marusu, amesema kuwa mpango huu wa mafunzo kazini kwa walimu, umekuja baada ya tafiti kubaini kuendelea kushuka kwakiwango cha elimu ya msingikulikochangiwa na ukosefu wa mafunzo ya uhakika kwa walimj wawapo kazini, hivyo QUEETS, ikajipanga kutoa mafunzo kwa walimu ili wawe mahiri katika ufundishaji wenye lengo la kutoa matokeo bora.

Awali shirika la HELVETAS kwa  kushirikiana na Chama cha Walimu Tanzania - CWT kupitia mradi wa Uboreshaji Elimu kwa Mpango wa Mwalimu Mahiri ( QUEETS), umeweza kutoa mafunzo kwa walimu 5514 kutoka shule za msingi 1,838, Maafisa Elimu wa kata 266 kwenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa kamati kuu ya Mradi wa kuwaendeleza walimu (QUEETS) ambaye ni mbunge wa Urambo, Mhe. Magreth Sita (kushoto) akizungumza na walimu walionufaika na mafunzo kazini wakati wa mkutano wa wadau wa elimu mkoani Arusha.


Walimu walionufaika na  Mradi wa kuwaendeleza walimu kazini (QUEETS) wakitoa shuhuda namna mradi huo ulivyowasaidia katika kubiresha ufundishaji wao, wakati wa mkutano wa wadau wa elimu mkoani Arusha.


Mwanafunzi wa Denis Elisa wa shule ya msingi Naurei akito ushuhuda wa namna mpango QUEETS ulivyowawezesha kushirikishwa na walimu wao na kuwasaidia kuelewa kwa njia  rahisi.


 Afisa Elimu Msingi, halmashauri ya arusha, mwalimu Hossein Mghewa akizungumza na kutoa ushuhuda namna mradi wa kuwaendeleza walimu kazini (QUEETS)  ulivyosaidia katika kuboresha ufundishaji ulioongeza ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba, wakati wa mkutano wa wadau wa elimu mkoani Arusha.


Wanafunzi wa shule ya msingi Naurei wakijifunza kwa makundi kwa kutumia zana rahisi zinazopatikana kwenye mzaingira yao.


Wanafunzi wa shule ya msingi Naurei wakijifunza kwa makundi kwa kutumia zana rahisi zinazopatikana kwenye mzaingira yao.


Wanafunzi wa shule ya msingi Naurei wakijifunza kwa makundi kwa kutumia zana rahisi zinazopatikana kwenye mzaingira yao.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.