Na. Elinipa Lupembe.
Wanafunzi wa kike shule ya sekondari Losinoni kata ya Oldonyowas, wameiomba serikali kuwajengea bweni ili waweze kulala shuleni, kutokana na changamoto inayowakabili ya kutembea umbali mrefu, kwenda na kurudi shuleni kila siku.
Wananafunzi hao wametoa rai hiyo, kupitia shairi waliloliimba mbele ya mgeni rasmi, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa kutoka kwa wadau wa maendeleo wa shule hiyo, hafla iliyofanyika shuleni hapo, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kupitia shairi hilo, wanafunzi hao, licha ya kuwashukuru wadau kwa misaada wanayoitoa kwenye shule hiyo, misaada ambayo inachochea maendeleo ya shule pamoja na wanafunzi kitaaluma, lakini walienda mbali zaidi na kuiomba serikali na wadau kuwajengea mabweni kwa kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi hao, wanaishi umbali mrefu kutoka shuleni hapo.
"Tunashukuru kwa misaada mingi inayotolewa na serikali na wadau, tunaomba mtufikirie zaidi, wenzenu tunatembea mpaka Kilomita 24, kwenda na kurudi shuleni, hili linakatisha ndoto za watoto wengi wa Losinoni, kwa baadhi yetu kuamua kuacha shule kwa kukata tamaa, na wakati mwingine wasichana huamua kuolewa, serikali yetu tunaomba mtusaidie ili watoto wa Losinoni nao wasome na kutimiza ndoto zao kama watoto wengine wa kitanzania" Walitoa ujumbe huo kupitia beti ya shairi lao
Wanafunzi hao, waliendelea kufafanua kwa hisia kubwa kuwa, wakati mwingine wanafunzi hunusurika kushambuliwa na wanyama wakali, kutokana na vijiji vyao kupitiwa na Korido ya wanyama pori, wanaotembea kati ya Hifadhi za Taifa za Arusha na Manyara na kuongeza kuwa, shule imezungukwa pia na makorongo makubwa, hivyo kipindi cha mvua inakuwa tatizo kwa wanafunzi kwenda na kurudi shuleni.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, alipokea ujembe huo kwa hisia sana, na kuahidi kufanyia kazi suala hilo, huku akiwaomba wadau wa maendeleo kujitokeza kuchangia ujenzi wa mabweni shule hiyo ya sekondari Losinoni.
"Watoto wangu, mmenipa ujembe huu, kwa hisia kali sana, mimi kama mzazi, nimelipokea tatizo na ninaahidi kwenda kulifanyia kazi kwa haraka ili tupate mabweni katika shule yenu na muweze kusoma na kutimiza ndoto zenu, niwapongeze kwa shairi lenu ambalo limebeba ujumbe mzito sana, kwa maslahi ya watoto wa kitanzania na Taifa kwa ujumla". Amesisistiza Mkurugenzi Msumi.
Shuel ya Sekondari ya Losinoni ni miongozpniwa mwa shuke za kata ilianzisjwa kwa nguvu za wananchi wa Kijiji cha Losinoni kwa ushirikiano na Hifadhi ya Taifa Arusha ANAPA, pamoja na halamshauri ya Arusha, na kuanza rasmi kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka mwaka 2016,
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.