• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANAFUNZI 1,073, 941 WAPANGIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 NCHINI

Posted on: December 14th, 2022

Na Elinipa Lupembe 

Jumla ya wanafunzi 1,073,941 nchini  waliofaulu Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2022 na kutangazwa na Baraza la Mitihani la TaTanzania wamepangiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka wa masomo 2023.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angela Kairuki, amesema kuwa jumal ya wanafunzi 1, 073, 941 wamefaulu na kupangiwa shule za serikali nchini.

Amefafanua kuwa idadi hiyo ya wanafunzi wavulana ni 514,846 na wasichana ni 559,095 ambao wote wanasifa stahiki ya kujiunga na masomo ya Sekondari katika shule za sekondari nchini.

Ameongeza kuwa idadi ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari, 2023 kwenye Shule za Sekondari 4,309 zimepangiwa wanafunzi ikiwa ni ongezeko la Wanafunzi 166,139 sawa na  asilimia 18.30, ikilinganishwa na Wanafunzi 907,802 waliopata alama za kuwawezesha kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka, 2022.

"Kati ya waliofaulu na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Kwanza wamo wanafunzi wenye mamahita, Maalum 2,775 sawa na asilimia 0.26 ambao kati yao Wavulana ni 1,491 na Wasichana 1,284". Amefafanua Mhe. Kairuki.

Hata hivyo Mhe. Wazri amebainisha kuwa mwaka huu kwa mara ya tatu, uchaguzi umefanyika kwa kutumia Mfumo wa Kielektroniki  'Students Selection- Management Information System' ulioundwa na wataalam wa TEHAMA wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Baraza la Mitihani la Tanzania, mfumo uliosaidia kupunguza muda, gharama pamoja na kuongeza ufanisi na uwazi, kuwa kila mwanafunzi anapangwa kwenye Shule kulingana na Mwongozo wa Uchaguzi unavyoelekeza.

Shule za Sekondari za Serikali walizopangiwa wanafunzi ni shule za Bweni na shule za kutwa, huku  upande wa shule za bweni, shule hizi zimegawanywa katika makundi matatu ambayo ni Sekondari za Bweni za Wanafunzi wenye ufaulu wa Juu zaidi (Special Schools), shule za sekondari za bweni za Ufundi na shule za Sekondari za Bweni za kawaida.

"Shule za Bweni ni za kitaifa na hivyo, zimepangiwa kupokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuzingatia mgawanyo wa nafasi uliobainishwa na vigezo vilivyowekwa ili kuimarisha Utaifa.

Aidha Waziri Kairuki ametumia fursa hiyo kuwapongeza wanafunzi wote waliowaliochag kujiunga na Kidato cha Kwanza na kuwashukuru Walimu, Wakuu wa Shule, Kamati za Shule, Maafisa Elimu Kata, Maafisa Elimu wa Halmashauri na Mikoa pamoja na Viongozi wote wa Halmashauri na Mikoa na Wadau wa Elimu nchini kwa kutoa ushirikiano katika kusimamia uendeshaji na utoaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari nchini.

Licha ya pongezi hizo Mhe. Waziri amewaasa wanafunzi wote waliochaguliwa kutumia vizuri fursa waliyoipata kusoma kwa bidii ili wafikie malengo waliyojiwekea na kutoa wito kwa viongozi wote kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaanza masomo yao mwezi 9 Januari, 2023 bila vikwazo vya aina yoyote ili kutekeleza azma ya Serikali ya utoaji wa Elimu msingi.

Ikumbukwe kuwa mwaka huu  hivyo kwa mwaka 2022,Mhe. Rais,  aliruhusu kukut fedha kiasi ha shilingi Bilioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 8,000 nchini kwa sjili ya ampokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.


ARUSHA DC 

KaziInaendelea ✍✍




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.