Na. Elinipa Lupembe.
Jumla ya wanafunzi 8, 075 wa darasa la saba, halamshauri ya Arusha, wanategemea kuanza mitihani yao ya Taifa ya kuhitimu darasa la saba mwaka 2020.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, akiwa ofisini kwake, Afisa Elimu Msingi, halmashauri ya Arusha, Mwl. Hossein Mgewa amesema kuwa wanafunzi hao 8,075 kutoka shule 134 za halmashauri ya hiyo, wanategemea kufanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2020 kwa mujibu ya ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzanzia (NECTA).
Amefafanua kuwa, kati ya watahiwa hao 8,075, watahiniwa 3,737 ni wavulana na watahiniwa 4,338 ni wasichana, na kuongea kuwa tayari maandalizi yamekamilika kwa watahiniwa wa shule zote 134 zikiwa za binafsi na za serikali.
Hata hivyo Afisa Elimu huyo, amewataka walimu na watakaohusika na zoezi la usimamizi wa Mtihani huo, kufuata kanuni, sheria na taratibu za Mitihani ya Taifa na kuepuka vitendo viovu, visivyokubalika na kanuni za Mitihani.
"Suala la Mitihani ni suala la Kitaifa, na zaidi ni suala nyeti sana, linalogusa maisha ya watu moja kwa moja, wasimamizi wa mtihani huu, wana jukumu la kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika kwa kuzingatia kanuni taratibu na maelekezo ya Baraza, ili wanafunzi hao wafanye Mitihani yao kwa amani na utulivu na kuweza kufikia malengo yao". Amesema Afisa Elimu Mghewa.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Sekei mwl. Adam Sambo, amesema kuwa, licha ya maandalizi ya Mtihani huo kukamilika katika shule yake, lakini Watahiniwa nao wamejiandaa vema, kufanya Mtihani huo ambao, walikuwa wakiusubiri kwa kipindi cha miaka 7 sasa.
"Watahiniwa wetu wameandaliwa vizuri na kwa muda mrefu, wako fiti kimwili, kiakili na kisaikolojia, na wako tayari kwa kufanya vizuri mtihani utakaonza kesho, zaidi tunategemea wanafunzi wote watafanya vizuri mitihani hiyo, kwa kuwa sio mtihani mgeni kwao, tulikuwa na utaratibu wa kuwapa mitihani ya majaribio, mara kwa mara" amefafanua Mwl. Sambo.
Hata hivyo, baadhi ya wanfunzi wa darasa la saba, halmashauri ya Arusha, wamethibitisha kujiandaa vema na mtihani huo wa Taifa, na kuweka wazi kuwa walimu wamewandaa vizuri kiakili na kisaikolojia, hivyo wanategemea kufanya vizuri katika mtihani huo wa Taifa na wanategemea kufaulu kwa kiwango cha juu.
"Mara kwa mara walimu wetu walitupima kwa majaribio ya mitihani ya Taifa iliyopita 'past papers', na kwa kufuata kanuni za mitihani, hivyo tunaamini mtihani huo hautakuwa mgeni kwetu, tunategemea kufanya vizuri na kupata ufaulu wa juu, kwa kuwa tumeandaliwa na sisi tumejiandaa vema" wamekiri wanfunzi hao
Awali uongozi wa Halmashauri ya Arusha, unawatakia kila la kheri wanafunzi wote wanaofanya mtihani wa Taifa Darasa la Saba 2020.
"MKAWE#KICHWA#NA#SI#MKIA"
#MATOKEO#CHANYA++
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.