• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANAFUNZI 8,075 WA DARASA LA SABA ARUSHA DC, KUFANYA MTIHANI WA TAIFA KESHO

Posted on: October 6th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.
     Jumla ya wanafunzi 8,075 wa darasa la saba, halmashauri ya Arusha, wanategemea kuanza mitihani yao ya Taifa kesho ya kuhitimu darasa la saba mwaka 2020 huku idadi ya wasichana ikiwa juu..

    Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake, Afisa Elimu Msingi, halmashauri ya Arusha, Mwl. Hossein Mgewa amesema kuwa, jumla ya wanafunzi  8,075 kutoka shule 134 za halmashauri ya hiyo, wanategemea kufanya Mtihani wa Taifa wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2020 kwa mujibu ya ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzanzia (NECTA).

       Amefafanua kuwa, kati ya watahiwa  hao 8,075,  idadi ya watahini wa wasichana ni 4,338 na watahiniwa 3,737 ni wavulana, na kuongea kuwa tayari maandalizi yamekamilika, kwa watahiniwa wa shule zote 134 zikiwa za binafsi na za serikali.

      Hata hivyo Afisa Elimu huyo, amewataka walimu na watakaohusika na zoezi la usimamizi wa Mtihani huo, kufuata kanuni, sheria na taratibu za Mitihani ya Taifa na kuepuka vitendo viovu, visivyokubalika na kanuni za Mitihani na Serikali kwa ujumla.

     "Suala la Mitihani ni suala la Kitaifa, na zaidi ni suala  nyeti  sana, linalogusa maisha ya watu moja kwa moja, wasimamizi wa mtihani huu, wana jukumu la kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika kwa kuzingatia kanuni taratibu na maelekezo ya Baraza, ili wanafunzi hao wafanye Mitihani yao kwa amani na utulivu na kuweza kufikia malengo yao". Amesema Afisa Elimu Mghewa.
      Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Sekei  mwl. Adam Sambo, amesema kuwa, licha ya maandalizi ya Mtihani huo kukamilika katika shule yake, lakini  Watahiniwa nao wamejiandaa vema, kufanya Mtihani huo ambao, walikuwa wakiusubiri kwa kipindi cha miaka 7 sasa.
     "Watahiniwa wetu wameandaliwa vizuri na kwa muda mrefu, wako fiti kimwili, kiakili na kisaikolojia, na wako tayari kwa kufanya vizuri mtihani utakaonza kesho, zaidi tunategemea wanafunzi wote watafanya vizuri mitihani hiyo, kwa kuwa sio mtihani mgeni kwao, tulikuwa na utaratibu wa kuwapa mitihani ya majaribio, mara kwa mara" amefafanua Mwl. Sambo.
    Hata hivyo, baadhi ya wanfunzi wa darasa la saba, halmashauri ya Arusha, wamethibitisha kujiandaa vema na mtihani huo wa Taifa, na kuweka wazi  kuwa walimu wamewandaa vizuri kiakili na kisaikolojia, hivyo wanategemea kufanya vizuri katika mtihani huo wa Taifa na wanategemea kufaulu kwa kiwango cha juu.
   "Mara kwa mara walimu wetu walitupima kwa majaribio ya mitihani ya Taifa iliyopita 'past papers', na kwa kufuata kanuni za mitihani, hivyo tunaamini mtihani huo hautakuwa mgeni kwetu, tunategemea kufanya vizuri na kupata ufaulu wa juu, kwa kuwa tumeandaliwa na sisi tumejiandaa vema"  wamekiri wanfunzi hao
     Awali uongozi wa Halmashauri ya Arusha, unawatakia kila la kheri wanafunzi wote wanaofanya mtihani wa Taifa Darasa la Saba 2020.
                         "MKAWE#KICHWA#NA#SI#MKIA"  
                                 #MATOKEO#CHANYA++




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.