Na Elinipa Lupembe.
Wanafunzi wa kidato cha sita halmashauri ya Arusha wametakiwa kuondoa hofu ya kupata maambukizi ugonjwa wa Corona, badala yake kuchukua tahadhari zinazoelekezwa mamlaka za afya, huku wakielekeza jitihada zaidi kwenye masomo, tayari, kwa kujiandaa na mitihani ya taifa inayotarajia kuanza tarehe 29, Juni 2020.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Elimu Sekondari, halmashauri ya Arusha, mwalimu Menard Lupenza, wakati alipotembelea baadhi ya shule za sekondari na vyuo, katika siku ya kwanza ya masomo, na kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha sita, mara baada ya serikali kufungua shule hizo.
Amesema kuwa, pamoja na changamoto ya ugonjwa wa Corona, maisha ya kila mtu lazima yaendelee na ndoto za wanafunzi hao lazima zitimie pia, huku akiwataka kutumia muda huu mfupi uliobaki, kujiandaa na mitihani kwa kusoma kwa bidii sambamba na wakijikinga na ugonjwa wa Corona.
"Tunaamini mambo mengi mlikuwa tayari mmefundishwa na mlikuwa mmnajianda na mtihani huu, fanyeni marudio ya mambo yote mliyofundishwa, sikilizeni walimu wenu, fuateni maelekezo yao bila kupoteza muda, hatimaye mtafaulu mitihani yenu ya mwisho" amesema Afisa Elimu huyo.
Aidha amewataka walimu na watumishi wa shule kujitoa kwa moyo kuwaelekeza na kuwasimamia wanafunzi kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona, kwa kuwasimamia kunawa mikono kila wakati huku wakiwafundisha kwa bidii, watieni moyo wanafunzi hawa, kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho.
Mkuu wa shule ya sekondari Ilboru George Otieno, amesema kuwa, jumla ya wanafunzi 120 kati ya 147 wameripoti shuleni hapo mpaka jana, na kukuta mazingira rafiki ya kujisomea yanayowezesha wanafunzi kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virus vya Corona.
Ameeleza kuwa tayari vifaa vya kunawia mikono vimewekwa maeneo yote muhimu, wanafunzi wote wamevaa barakoa, wamepunguza idadi ya wanafunzi darasani kwa kukaa umbali wa mita moja kati ya wanafunzi mmoja na mwingine pamoja na kutenga dakika 30 za kufanya mazoezi kila siku.
Christopher Kaduma, mwanafunzi wa kidato cha sita, ameishukuru serikali kwa kuweka mazingira salama ya kujifunzia, jambo ambalo limewaondoa hofu na kujengewa hali ya kujiamini na kuahidi kutumia muda huu mfupi kujiandaa na mitihani ya taifa huku akiwa na imani ya kufaulu kwa kiwango cha juu.
Hata hivyo ziara Afisa Elimu huyo aliambatana na Maafisa Afya na Afisa Ustawi wa jamii, waliwaelekeza wanafunzi namna bora ya kunamikono pamoja na kutoa ushauri wa kuwa sawa kisaikolojia.
Afisa Elimu Sekondari, halmashauri ya Arusha, akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita, shule ya sekondari Bishop Danning, na wanachuo cha Ualimu Bishop Dunning, kata ya Moivo.
Wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Bishop Danning, na wanachuo cha Ualimu Bishop Dunning kata ya Moivo, wakisikiliza maelekezo ya Afisa Elimu na watalaam wa Afya siku ya kwanza ya kufungua shule.
Wanafunzi wa kidayo cha sita shule ya sekondari Ilboru, wakisikiliza maelekezo ya Afisa Elimu na watalaam wa Afya siku ya kwanza ya kufungua shule.
Afisa Afya na Elimu Shuleni, halmashauri ya Arusha, Niah Mtaki, akiwaelekeza wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Bishop Dan, namna bora ya kunawa mikono.
Wanafunzi wa kidayo cha sita shule ya sekondari Winning Spirit, wakisikiliza maelekezo ya Afisa Elimu na watalaam wa Afya siku ya kwanza ya kufungua shule.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.