• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wanafunzi Mwandeti sekondari kuanza kutumia bwalo la chakula

Posted on: March 11th, 2019

Wanafunzi shule ya sekondari Mwandet, halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru,  wanategemea kuanza kutumia bwalo lao la chakula, baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi bwalo hilo, bwalo ambalo wanafunzi  hao wamekuwa wakilisubiri kwa muda mrefu.

Wanafunzi hao, ambao kwa sasa hawana sehemu maalumu ya kulia chakula, jambo ambalo linawapa usumbufu mkubwa kwa kula chakula nje wakiwa wamesimama au kukaa katika maeneo yasiyo rasmi kwenye maeneo ya shule.

Akizungumza na mwandishi wetu, alipotembelea shuleni hapo, mkuu wa shule ya sekondari Mwandet, mwalimu John Masawe, amesem kuwa, wamepokea fedha kutoka Serikali Kuu, za miradi ya P4R, kiasi cha shilingi milioni 100, fedha ambazo kiasi cha shilingi milioni 50 kinatumika kumalizia ujenzi wa bwalo la chakula huku milioni 50 nyingine zikianzisha ujenzi wa maktaba.

Mwalimu Masawe amekiri kuwa, ukamilishaji wa bwalo hilo la chakula, utaondoa adha kubwa wanayoipata wanafunzi wakati wa kula, kwakuwa husimama na kukaa nje, mazingira amabyo si rafiki wala salama kiafya, kutokana na hali ya hewa ya eneo hilo ya upepo unaombatana na vumbi, wakati wa jua na baridi kali na wakati wa mvua pia, hali zote huwapa usumbufu mkubwa wanafunzi hao.

Ameongeza kuwa, licha ya kuwa hali ya hewa ni changamoto kubwa, kitendo cha kulia nje kinaenda sambamba pia na uchafuzi wa mazingira, jambo ambalo linatishia usalama wa wanafunzi kiafya.

Hata hivyo mwalimu Masawe, amethibitisha kuwa, fedha hizo zinatosha kutakamilisha ujenzi wa bwalo hilo na wanategemea likamilike na kuanza kutumika mapema mwishoni mwa mwezi Machi kwa kuwa fundi anayefanya kazi hiyo anakwenda vizuri.

Amezitaja kazi zinazofanyika ni pamoja na uwekaji wa sakafu na malumalu, milango na madirisha, upakaji wa rangi kwa jengo zima, uwekaji wa majiko matatu ya kisasa pamoja na meza na viti vya kukalia wanafunzi hao wakati wa kula.

Salhat Adam, mwanafunzi wa kidato cha kwanza anashukuru serikali kwa kuwajengea bwalo, kutokana na adha wanayoipata kwa kula chakula nje, jambo ambalo linatishia usalama wa afya zao.

Akizungumzia upatikanaji wa chakula shuleni hapo, mkuu huyo wa shule amesema kuwa, kwa wanafunzi wa bweni wa kidato cha tano na sita serikali inatoa chakula, kwa wanafunzi wa  kidato cha kwanza mpaka cha nne wa bweni na kutwa, wanagharamiwa na wazazi  kwa makubaliano ya wazazi wenyewe.

Hata hivyo, mkuu huyo wa shule, amesema kuwa bado kuna changamoto kwa wanafunzi wa kutwa, ambao baadhi ya wazazi kushindwa kuchangia chakula cha watoto wao, na kuwasababishia watoto hao kushinda na njaa wawapo shuleni.

Amewataka wazazi hao kujitoa, kuwalipia watoto wao fedha ya chakula kwa kuwa licha ya kuwa ni jukumu lao, lakini ni kwa ajili ya afya na maendeleo ya watoto wao, kutokuwalipia ni kuwanyanyasa kisaikolojia, hata maendeleo yao darasani huwa ni ya kusuasua.

"Wazazi waoneeni huruma watoto wenu, walipieni chakula, mtoto anakaa shuleni muda mrefu na njaa, anapoona wenzake wanakula yeye hali, ananyanyasika sana, hata maendeleo yake darasani yanasuasu. Amesema Mwalimu Masawe.

Shule ya sekondari Mwandet ilianza mwaka 2004, na mwaka 2016 ikipandishwa hadhi na kuwa na kidato cha 5 na 6, na ina jumla ya wanafunzi 1,232 kidato cha kwanza mpaka cha sita.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.