Na Elinipa Lupembe
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mringa, halmashauri ya Arusha wameishukuru serikali kwa kuwajengea abweni mapya pamoja na kukarabati mabweni ya zamani yaliyokuwa yamechakaa shuleni hapo, ujenzi unagharimu kiasi Cha shilling million 360 fedha kutoka serikali kuu kupitia mradi wa SEQUIP.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wanafunzi shuleni hapo, wameeleza furaha waliyonayo kutokana na kuongezewa mabweni mapya na kukarabatiwa yale ya zamani kuwa, uwepo wa mabweni hayo licha ya kuwa na sehemu bora ya kulala itaongeza ari ya kusoma na kuongeza ufaulu wao, usalama wa wanafunzi na mali zao, kuondoa utoro pamoja na kuondoa hofu waliyokuwa nayo ya kuambukizana magonjwa kutokana na msongamano na kuwafanya kuishi kwa nafasi sasa.
Christine Mkama mwanafunzi wa kidato cha sita ameishukuru serikali ya mama Samia kwa kujenga mabweni hayo ambayo wa amekiri kuamini kuwa mabweni hayo, yatawawezesha wanafunzi kuishi kwa nafasi kulingana na idadi yao pamoja na kuongeza ari ya kusoma na ufaulu pia.
"Tunaishukuru serikali, tunamshukuru mama Samia kwa kuendelea kutujali wanafunzi hasa wasichana na kuona umuhimu wa kutujengea mabweni mapya, mabweni pamoja na usimamizi mzuri wa walimu yanatupa hamasa ya kusoma vizuri na kufaulu mitihani yetu" Amesema Christine.
Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi Grace John, amebainisha kuwa na upungu wa mabweni shuleni hapo, uliosababisha baadhi ya wanafunzi kuwa na ufaulu wa chini, na kuongeza kuwa mapinduzi yaliyofanywa na serikali ya mama Samia, yatawapa nafasi nzuri ya kujisomea na kuweza kufaulu zaidi.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Mringa Mwl. Salim Magaka, amesema kuwa shule ilipokea shilingi milioni 360, milioni 260 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili huku million 100 zikiwa ni za ukarabati wa mabweni manne na matundu ya vyoo, mabweni ambayo yalikuwa yamechakaa sana kutokana na kujengwa kwa miaka mingi iliyopita.
"Mabweni haya yote ni kwaajili ya wanafunzi wa kike na kukamilika kwake tunategemea kupunguza msongamano mabwenini na utakaochochea ari ya wanafunzi kujisomea na kuwezesha ufaulu kuongezeka". Mwl. Magaka
Awali Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu halmashauri ya Arusha, Anna urio ameongeza kuwa halmashauri ya Arusha imepokea shilingi bilioni 1.4 fedha za mradi wa SEQUIP kwa ajili ya kutekeleza miradi elimu sekondari na kufafanua kuwa milioni 360, ujenzi na ukarabati wa mabweni shule ya sekondari Mringa, milioni 580.3 ujenzi wa shule mpya ya sekondari Moivo na milioni ikiwa ni ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya sekondari Kiutu
"Tunatemea kukamilika kwa miradi yote, kutafikia lengo la serikali la kuboresha miundo mbinu ya shule nchini la kuwezesha mazingira bora ya kujifunzia, kuwezesha idadi kubwa ya watoto wa kitanzania kupata fursa ya elimu na kutimiza ndoto zao za kielimu hata kuwafikia watoto ambao wazazi wao hawakuwa na na uwezo wa kuwasomesha watoto wao" Amesema Anna.
Ujenzi na ukarabati wa miradi hiyo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2023.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.