Na Elinipa Lupembe.
Kiongozi wa mbio Mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 Kitaifa, Luteni Josephine Paul Mwambashi, amewataka wananchi wa Arumeru, kuacha kutumina vibaya, teknolojia ya Habari na mawasiliano TEHAMA, badala yake kuitumia vema teknoljia ambayo ina kasi kubwa ya katika kuharakisha maendeleo ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Kitaifa, amesema hayo, wakati akitoa ujembe wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru 2021, zilipotembelea na kukagua jumla ya miradi tisa ya maendeleo katika wilaya ya Arumeru, yenye halmashauri mbili za Arusha na Meru.
Ameweka wazi kuwa, kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknoloji duniani sasa, TEHAMA ikitumika vizuri, inauwezo mkubwa wa kuleta maendeleo katika sekta zote muhimu, huku akiwasisitiza vijana, kujikita kujifunza matumizi ya teknolojia hiyo ya mawasiliano, teknolojia ambayo dunia imejielekeza huko.
TEHAMA inarahisisha kufanyika kwa kazi mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato, na kuzitaka halamshauri kukusnaya mapato kwa kutumia mashine, huku akiwasisitiza wafanya biashara kutumia mashine za EFD, na kuwakumbusha wananchi kuhakikisha wanachukua risiti pindi wanapofanya manunuzi.
Hata hivyo Kiongozi huyo wa Mwenge wa Uhuru kitaifa, licha ya kuwataka wananchi kutumia TEHAMA kwa maendeleo, amewasistiza pia wananchi kujihadhari na vitendo vya rushwa, kwa kuwa rushwa ni kinyume na haki za binadamu na inarudisha nyuma maendeleo.na kuongeza kuwa afya ya kila mtu ni muhimu hivyo kujikinga na magonjwa ya Malaria na UKIMWI.
Aidha Kiongozi huo wa Mwenge wa Uhuru kitaifa Lutwn Josephine, hakuacha kuwasisistiza wananchi, kujali afya zao kwa kuzingatia lishe bora, lishe amabayo inawafanya wananchi kuwa na afya bora kwa ajili ya ujenzi wa taifa la Tanzania.
Mwenge wa UHURU 2021 umekimbizwa umbali wa Kilomita 126.3 katika halmashauri zote mbili, kutembelea jumla ya miradi tisa (9) yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3 katika sekta ya Afya, Elimu, Maji, Barabara na Uwekezaji.
Mwenge huo Maalumu wa Uhuru 2012, umefanya shughuli za kuzindua mradi wa TEHAMA shule ya msingi Mlangarini, mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Kikwe na mradi wa jengo la mama na mtoto hospitali ya wilaya ya Olturumeti na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa mradi barabara Sangisi - Nambala, mradi wa kusukuma maji Losikito pamoja na mradi wa Kituo cha Mafuta Africa Petrol kata ya Oloirieni.
Aidha Mwenge Maalum wa Uhuru 2021, umetembelea na kukagua mradi wa shamba la migomba na tumbaku kata ya Olturumeti, miundombinu ya wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi Ilboru na kukamilsha kwa kutembelea mradi wa Kikundi cha vijana -Umoja Youth Group kata ya Moivo.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2021 “TEHAMA ni Msingi wa Taifa endelevu; itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.