• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi wa Mbuyuni kata ya Oljoro wapata matumaini ya kupata umeme tangu Uhuru wa Tanganyika

Posted on: March 20th, 2018

Matumaini ya kupata nishati ya umeme yawashukia wananchi wa Mbuyuni kata ya Oljoro baada ya kusubiri nishati hiyo tangu kupatikana kwa  Uhuru wa Tanganyika zaidi ya miaka hamsini iliyopita. 

       Matumaini hayo yakwenda mbali zaidi, baada ya Waziri mwenye dhamana kuagiza na kusisitiza nishati hiyo ya umeme uwafikie wananchi wote kwa kuzingatia kijiji kwa kijiji, kitongoji kwa kitongoji na hadi nyumba kwa nyumba.    

     Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema hayo alipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa umeme vijiji unaotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini - REA katika eneo la Mbuyuni, halamshauri ya Arusha  wilayani Arumeru.  

      Waziri Kalemani ameliagiza shirika la umeme TANESCO kupitia wakaka wa umeme vijijini-REA kuwaunganishia umeme wananchi wote bila kujali hadhi za nyumba zao wanazoishi.       

      Amesisitiza kuwa umeme uwekwe kwa mwananchi yoyote anaehitaji na mwenye uwezo wa kulipia gharama za kuunganisha hata kama nyumba yake ni ya udongo na kuezekwa kwa nyasi.     

      "Sitaki kusikia mneacha nyumba ya mtu kwa sababu hali duni ya nyumba, hali ya nyumba ya mtu haiwahusu" amesisitiza Waziri Kalemani.  

 Aidha amewataka wananchi hao kulipia gharama za kuunganishiwa umeme kiasi cha shilingi 27,000 tu na kuongeza kuwa endapo mtu atatozwa zaidi, atoe taarifa kwa viongozi wa  ngazi ya wilaya na mkoa. 

      Hata hivyo Waziri huyo ameagiza umeme uunganishwe ndani ya siku saba baada ya mwananchi  kukamilisha taratibu za malipo, na kuwataka wananchi kulinda miundombinu ya umeme katika maeneo yao na kujenga uzio kwenye transfoma. 

         Meneja wa TANESCO mkoa wa Arusha Gasper Msigwa amesema kuwa REA III kwa kipindi cha awamu ya kwanza itawaunganishia nishati ya umeme wateja wapatao 6,000 katika maeneo 58 ya mkoa wa Arusha, mradi utakao gharimu shilingi bilioni 9.3. Ameeleza kuwa hadi sasa jumla ya wateja 1,652 wamekamilisha taratibu za malipo na tayari miundombinu ya umeme imeksmilika kwa aslimia 90%. 

     Msigwa ameongeza kuwa, licha ya juhudi hizo za serikali ya awamu ya tano, bado shirika linakabiliwa na changamoto ya wizi wa nyaya za umeme na baadhi ya watu kukosa uaminifu na kujiunganishia umeme bila kufuata taratibu.  

      Loth Sabaya mkazi wa Oljoro amesema kuwa  wamefurashwa na neema nishati ya umeme kijijini kwao, na kuongeza kuwa kukosa umeme kunawacheleweshea maendeleo,na wanashindwa kufanya shughuli za uzalishaji zinahitaji nishati ya umeme.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.