Wananchi wa Kijiji cha Bwawani Kata ya Bwawani, wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajengea Vyumba vitatu vya madarasa na matundu matatu ya vyoo shule mpya ya msingi Olokii na kuondoa changamoto ya uhaba wa vymba vya madarasa uliyokuwa inaikabili shule hiyo.
Wananchi hao wamefurahishwa sana na Ujio wa Mradi huo ambao unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 75 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa fursa sawa katika Ujifunzaji bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu kwenye shule 6 za msingi za halmashauri ya Arusha ambapo shule hiyo ilikuwa na vyumba viwili tu vya madarasa.
Akizungumza na mwandishi wetu wakati ujenzi wa Mradi huo unaanza, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Sarianda Sikoi amesema kuwa mradi huo utaleta tija kubwa kwa wakazi wa Kijiji hicho kwani watoto watapata fursa ya kusoma kwa uhuru kwasababu changamoto hiyo ya upungufu wa vyumba vya madarasa itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa hali itakayopelekea shule hiyo kuwa na uhaba wa vyumba viwili vya madarasa.
Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali pamoja na wafadhili wa Mradi huo na kuiomba Serikali kuendelea kutupia macho katika shule hiyo na kuwajengea nyumba za walimu ili waweze kuishi karibu na shule kwani walimu wananishi mbali na eneo la shule.
“Tunaomba Serikali itujengee nyumba za walimu kwasababu kwa kipindi hiki tuna nyumba moja tu ya mwalimu mkuu na walimu wengine wanaishi kwenye nyumba za wakazi wanaotuzunguka”. Amesema Mwalimu mkuu huyo.
Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Olmapinu, Mhe. Lazaro Mathayo amebainisha kuwa mazingira ya watoto wa kitongoji hicho yalikuwa magumu hasa kwa watoto kwani walilazimika kutembea umbali mrefu Kwenda shule jirani hivyo ujio wa Mradi huo utasaidia watoto wa jamii hiyo kuondokana na ujinga na kufikia malengo ya Serikali kwaajili ya Watanzania wote.
Aidha, wanafunzi wa shule hiyo nao wameishukuru Serikali kwa kuwaletea mradi huo ambao utawapa fursa ya kupata elimu kama watoto wengine na kuwasaidia kutimiza ndoto zao.
“Tunaishukuru Serikali kwa kutukumbuka na kutujengea madarasa, hapo awali tulikuwa tunapata shida ya kutembea umbali mrefu lakini sasa tutasoma vizuri tukiwa darasani badala ya kusomea nje”. Alisema mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Faiza Omary.
Awali, Halmashauri ya Arusha ilipokea kiasi cha shilingi milioni 682.5 kutoka Serikali Kuu kwaajili ya kutekeleza miradi hiyo katika shule sita za msingi halamsahuri ya Arusha.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
KaziInaendelea
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.