Na Elinipa Lupembe
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, ameongoza zoezi la upandaji Miti, katika viwanja vya shule mpya ya sekondari Kijiji cha Olkokola kata ya Lemanyata ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya upandaji miti mwaka 2023.
Mkurugenzi Msumi ameelezea hali ya uharibifu wa mazingira uliokithiri nchini, huku madhara yake yakianza kujidhihirisha wazi, kutokana na hali ya ukame inayosababbishwa na ukosefu wa mvua na maeneo mengine mvua kubadili misimu yake.
Amesema kuwa Serikali imejipanga kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, kwa kuwaelimisha na kuhamasisha jamii kupanda miti, kwa kuhakikisha wananchi wote wanapanda miti kwenye maeneo yate yanayowazunguka, ikiwemo nyumbani, kwenye taasisi za Umma na binafsi pamoja na kuitunza miti hiyo.
Aidha amewasisitiza wananchi wote kuhakikisha wanaungana na Serikali katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yote yanayowazunguka pamoja na kuitunza.
"Miti tuliyoipanda tunatakiwa kuitunza mara nyingi Serikali inatoa miti na kufanya Kampeni za upandaji miti, lakini utunzaji unakuwa hafifu, hivyo ni jukumu letu kusimamia utunzaji wa miti iliyopandwa kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo". Amesisitiza Msumi.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Olkokola Mhe. Thomas Meirura, ameahidi kuwasimamia wananchi wote kupanda miti kwenye maeneo ya wazi, mashamba na nyumbani pamoja na utunzaji wa miti hiyo.
"Tunashukuru Serikali kutuletea miti, kuna maeneo yamekatwa miti sana, hivyo tunakwenda kupanda miti hii, na kuhakikisha inakua kwa manufaa yetu, tumefahamu umuhimu wa miti kwenye mazingira yetu, tuaahidi kuitunza" Ameeka wazi Mwenyekiti .
Awali Afisa Programu ya wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima na Wafugaji mkoa wa Arusha ( MVIWAARUSHA), Damian Sulumo, amesema kuwa taasisi yao imeandaa mpango wa kupanda miti kwenye vijiji 8 vya halmashauri ya Arusha kwa awamu ya kwanza.
Mti wangu, Taifa langu, Mazingira yangu, KaziIendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.