Na. Elinipa Lupembe.
Wananchi walioingizwa kwenye mpango wa mradi wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF awamu ya IV, halmashauri ya Arusha, wameishukuru serikali na kumpongeza mama Samia, kwa kuwajali kinamama na wazee wa kijiji hicho.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wakati wa zoezi la kupokea fedha za ruzuku za awamu mbili, wananchi wa kijiji cha Lemanda, wamemshukuru mheshimiwa Rais mama Samia na serikali ya awamu ya sita, kwa kuwaingiza kwenye mpango huo, kwa kuwa kijiji hicho hakikuwemo kwenye mpango kwa awamu zilizopita.
"Tunaishukuru serikali kwa kutujali wananchi wa Lemanda, tulikuwa tunakabiliwa na hali ngumu ya maisha, tunaahidi kuanzisha vikundi vidogo vidogo vya ujasiriamali, ili kufanya biashara, tunaahidi hatuamuangusha mama, hela ya mama Samia itupe mafanikiao kwenye familia zetu". Amesisistiza Nshooki Marko.
Naye Upendo Joseph, licha ya kuishukuru serikali amesema kuwa, tangu wameanza kupokea fedha hizo, tayari wameanza kuona mafanikio yake, kutokana na kuanzisha miradi midogo midogo ya kufuga kuku na kuuza mboga mboga, miradi ambayo imeanza kuwawezesha kuapata fedha ya kujikimu kimaisha.
Diwani wa kata Oldonyosambu, Mhe. Raymond RLairumbe, ameweka wazi kuwa, wananchi wa Oldonyosambu wameridhishwa na kufurahishwa na kitendo cha serikali kuwaingiza, kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini mradi unaotekelezwa na TASAF awamu ya IV, na kujioana na wao wamekuwa sawa na wanatanzania wengine, ambao walikuwa wakipokea ruzuku ya fedha kutoka serikalini.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Lemanda, Mosses Kalomba, amefafanua kuwa, wao kama viongozi wataendelea kuwasimamia wanufaika hao wa TASAF, kutumia fedha hizo vizuri kwa kufanya biashara ndogo ndogo ili kuinua uchumi na pato la familia, na kuongeza kuwa tayari wamewahamasisha wanufaika hao, kujiunga na BIMA ya Afya iliyoboreshwa ili weweze kuwa na uhakika wa kupata matibabu pindi wanapougua.
Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amewataka wanufaika hao wa TASAF, kutumia vizuri fedha wanazopokea kwa kufanya biashara na kuanzisha miradi midogo midogo katika maeneo yao, ili kujikwamua katika hali ya umasikini uliokuwepo.
"Tujitahidi kutumia fedha tunazopewa na serikali vizuri ili kujikwamua na hii ya umasikini pamoja na kuhakikisha tunaboresha hali zetu za kimaisha" amesisitiza Mkurugenzi Msumi.
Awali Mratibu wa TASAF, Halmashauri ya Arusha, Grace Makema, amesema kuwa jumla ya shilingi bilioni 1.178, zimetolewa na kuhawilishwa kama ruzuku kwa jumla ya kaya 14,135 kwenye vijiji 88 vya halmashauri ya Arusha kwa awamu mbili za mwezi Novemba na Desemba na Januari na Februari 2022.
Ikumbukwe kuwa, katika mradi wa TASAF awamu ya III jumla ya vijiji 45 vilikuwa kwenye mpango, na katika mradi wa TASAF awamu ya IV vijiji vingine 39 vimeingizwa kwenye mpango na kufanya vijiji vyote 88 vya halmashauri ya Arusha vimeingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍✍
Wananchi wa kijiji cha Lemanda wakisubiri kupokea ruzuku ya fedha, zinazotolewa na serikali kupitia mradi wa TASAF awamu ya IV.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.