Na Elinipa Lupembe
Wananchi husussani kina mama halmsahuri ya Arusha wamejitokeza kuadhimisha siku Saratani ya Matiti Duniani 2022 Iiliyofanyika kwenye hotel ya Olarndo Garden eneo la Sakina..
Kina mama hao licha ya kupata ufahamu na kupima bure Saratani ya Matiti na Mlango wa Kizazi, bure pamoja na magonjwa yasiyoambukiza, pia walipata fursa ya kupata elimu ya changamoto ya Afya ya Akili.
Katika dunia ya sasa watu wengi wanakabiliwa na changamoto ya afya ya akili bila kujifahamu na kujikuta wakipoteza mwelekeo wa maisha na kutengwa na ndugu, jamaa na marafiki.
Mratibu wa Afya ya Akili halmashauri ya Arusha, Dkt. Pascal Kang'ria, amefafanua kuwa changamoto ya afya ya akili matokeo ya sonona kali inayosababishwa msongo wa mawazo unaotokana na hali anazopitia mtu katika maisha yake ya kila siku.
Mara nyingi mtu mwenye changamoto ya Afya ya Akili huwa hajitambui kama ana tatizo, kwa kuwa wengi wao hujitenga na watu wao wa karibu na pengine kufanya vitu tofauti anavyohisi vinampa ahueni yeye bila kujali madhara yake kwa wengin
Kutokana na hali hiyo watu waliomzunguka kwa kutokujua tatizo lake, huanza kumshambulia na kumuona ana tabia zisizofaa, jambo ambalo humpoteza kabisa na wakati mwingine humsababisha hata kujiua.
Aidha Dkt. Kang'iria ameitaka jamii kufahamu dalili za changamoto ya Afya ya Akili kwa mtu binafsi na watu wao wa karibu ili kuweza kuzishughulikia kwa njia sahihi kwa bali kuzitatua kupitia tabia na mienendo ya mtu na jamii.
Amezitaja sababu za kawaida zinazomfanya mtu kupata changamoto ya akili ni pamoja na hali duni ya maisha, ukatili wa kingono utotoni, uonevu, ukosefu wa usawa kiuchumi na kijamii, unyanyapaa, ubaguzi na ukiukwaji wa haki za binadamu hususani kwenye maeneo ya kazi.
Aidha Dkt. Kang'iria ameweka wazi njia sahihi za kuepuka changamoto ya akili ni pamoja na kujikubali, kufahamu kuna kushinda na kushindwa, kuacha kuficha siri bali kuwa na mtu wa kumueleza siri zako, kutokukaa kimya, kuongeza marafiki, kupata muda wa kupumzika hasa kulala, na kufanya yale unayoyapenda, kujipa raha mwenyewe pamoja na kutoka na marafiki.
Inafahamika kuwa changamoto ya Afya ya Akili inaongezeka mwaka hadi mwaka, matokeo ya tafiti ya mwaka 2019, takribani watu bilioni 1 huku asilimia 14 ya vijana barurbaru duniani wanaishi na tatizo la akili, tatizo lilisababisha mtu 1 kati ya 100 kujiua na asilimia 58 ya watu wanaojiua ni watu wenye umri wa chini ya miaka 50.
Hata hivyo WHO inasema tatizo la akili ni sababu inayoongoza watu kupata ulemavu duniani, watu wenye tatizo la akili hufariki dunia miaka 10 hadi 20 mapema zaidi kuliko watu wa kawaida kutokana na magonjwa ya mwili yanayoweza kuzuilika.
Awali Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na shirika la LUMINARY INC wamefanya Maadhimisho ya Wiki ya SARATANI YA MATITI Duniani 2022 yenye Kauli mbiu: "UTAMBUZI WA MAPEMA HUOKOA MAISHA", kwa kutoa huduma za upimaji bure kwa magonjwa yasiyoambukiza na yanayoambukiza ikiwemo Saratani ya Matiti na Saratani ya Shingo ya kizazi kwa siku tatu kuanzia tarehe 27-19 Oktoba 2022.
ARUSHA DC
KaiInaendela✍
PICHA ZA MATUKIO WATU WAKIPATA ELIMU YA CHANGAMOTO ZA AFYA YA AKILI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.