Wananchi wakazi wa kata ya Nduruma halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wamejitoa kuchangia fedha za kujenga choo kwa ajili ya watumishi wa kituo cha Afya Nduruma ambao wamehama kwenye nyumba hizo kutokana na nyumba hizo kukosa vyoo.
Wananchi hao wamefikia uamuzi huo baada ya kuthibitisha tabu inayowakabili watumishi hao wanaolazimika kuishi mbali na kituo hicho na kusababisha utendaji wao kazi kulegalega jambo linalosababisha pia upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi hao kusuasua.
Akizungumzia hatua hiyo Kaimu Muuguzi Mkuu halmashauri ya Arusha Sista Agusta Komba amesema kuwa fadha hizo zimechangwa na wananchi wa Nduruma, watumishi wa idara ya Afya kwa kushirikiana na shirika la InGender Health na kupata kiasi cha shilingi milioni moja kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa choo hicho.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.