• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi watakiwa kujenga tabia binafsi ya kunawa mikono kwa kufuata hatua sahihi

Posted on: October 15th, 2018

Wananchi katika halmashauri ya wilaya ya Arusha, wilayani Arumeru, wametakiwa kunawa mikono kwa kuzingatia kanuni na hatua sahihi za unawaji mikono, kwa kutumia maji safi na sabuni ili kujikinga na magonjwa yatokanayo na uchafu wa mikono.  

Rai hiyo imetolewa na  mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Kunawa Mikono Duniani, Afisa Usafishaji na Mazingira, halmashauri ya Arusha, Vanika Ndelemu, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, yaliyofanyika kwenye viwanja vya kanisa la KKT Usharika wa Ilkiding'a.

Afisa Usafishaji huyo, amesema kuwa, endapo wananchi watazingatia kanuni sahihi za unawaji mikono, wataondokana na magonjwa, yanayotokana na uchafu wa mikono na kufanya bajeti ya dawa inayotumika kutibu magonjwa hayo,  kuweza kutumika kutatua changamoto nyingine zinazowakabili wananchi.

Ameongeza kuwa, magonjwa yanayotokana na uchafu wa mikono, yanaepukika na hayapaswi kuwepo katika familia na jamii zetu, hivyo ni vyema kujipanga kuyapiga vita kwa kuchukua tahadhari binafsi kwa kunawa mikono kwa kutumia maji safi na sabuni.  

" Kwa mwaka huu wa fedha 2018/19 halmashauri imepanga kutumia shilingi milioni 861.2 kwaajili ya kununulia dawa  na vifaa tiba, endapo tutajikinga na magonjwa yatokanayo na mikono michafu, sehemu ya fedha hizo iingetumika, kuimarisha miundo mbinu ya barabara na maji pamoja na shughuli nyingine" amefafanua Mgeni rasmi huyo.

Aidha, amewaagiza Maafisa watendaji wa kata na vijiji kusimamia, uundaji wa Kamati za ufuatiliaji wa hali  ya vyoo na unawaji wa mikono, kwa kutumia vibuyu chirizi vyenye maji safi na sabuni, na kuhakikisha taasisi zote na kaya zote zinakuwa na vyoo vyenye vifaa hivyo.  mikono.

 "Simamieni taasisi zote na wananchi katika maeneo yenu, na kuhakikisha maeneo yote yana vyoo bora na si vyoo pekee bali vyoo vyenye vifaa vya maji yanayotiririka na sabuni ili kila mtu aweze kunawa mikono mara baada ya kutoka chooni" amesisitiza Ndelemo.

 Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi,  Afisa Afya halmashauri ya Arusha, Issa Msumari, amesema kuwa, licha ya kuwa, kwa sasa hali ya uwepo wa vyoo imeimarika kwa zaidi ya asilimia 90, lakini takwimu za hali ya unawaji mikono katika halmashauri hiyo, ni asilimia 35 tuu, jambo ambalo linatishia hali za afya na uwepo wa magonjwa ya kuhara, kuhara damu, magonjwa ya macho, magonjwa ya ngozi, maambukizi ya mfumo wa hewa yanayosababisha mafua  pamoja na homa ya mapafu.        

Awali maadhimisho hayo yaliambatana na burudani za vikundi  mbalimbali  zenye jumbe za uhamasishaji wa unawaji mikono, burudani zilizokwenda sambamba na masindano ya vikundi hivyo, ambayo kikundi cha maigizo, kutoka shule ya msingi Olchoki na Natema, waliibuka kidedea na kupata zawadi ya shilingi laki moja na elfu hamsini, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na shule ya kimnyaki na Selian, na nafasi ya tatu kuchukuliwa na shule ya msingi  Loruvani na Moivo na washindi wa pili na watatu wote kupata fedha taslimu shilingi elfu hamsini.      

Hata hivyo jumla ya shule za msingi 20 zimetunukiwa vyeti vya ushiriki katika maadhimisho hayo, kwa kuyapamba na kuwezesha wanafunzi na jamii iliyohudhuria, kufahamu umuhimu wa unawaji mikono unaozingatia hatua sahihi.   

Uongozi wa Halmashauri ya Arusha, unawataka wadau mbalimbali kujitokeza kuhamasisha na kuwajengea wananchi uwezo wa umuhimu wa unawaji mikono na kuwashukuru wadau wa mashirika ya SNV, AceAfrica, WaterAid na Root&Shoots kwa kufanikisha maadhimisho hayo pamoja na kutoa elimu za afya ya jamii,  katika halmashauri hiyo.

 Maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani, hufanyika Oktoba 15  kila mwaka, maadhimisho yaliasisiwa  na shirika la Afya duniani (WHO) mwaka 2008, kwa mara ya kwanza Tanzania iliadhimisha mwaka 2011, kwa lengo la kuhamasisha,  jamii kuongeza uelewa na ufahamu zaidi, umuhimu wa unawaji mikono kwa maji tiririka na sabuni.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.