Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, anawatangazia wananchi wote wenye viwanja vilivyopimwa ndani ya mipaka ya halmashauri hiyo, kulipa Kodi ya Ardhi kabla ya tarehe 30.05.2018.
Kadhalika wamiliki wote wa viwanja katika eneo la Endurace (Kivulini ) lilipokuwa shamba namba 181/3/2 wanatakiwa kufika ofisi za Ardhi chumba Na. 3 ili kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 30/05/2018, kutokulipa kodi kutasababisha kupelekwa Mahakamani na viwanja vyao kuuzwa.
Kwa wale wote waliotumiwa Hati ya Madai (Demand Notes ) wanatakiwa kulipa kabla ya tarehe hiyo, endapo tarehe hito itapita watapelekwa Mahakamani.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.