Na Elinipa Lupembe.
Wanawake walio kwenye mpango wa Kunusu kaya masikini kijiji cha Ilkiding'a, wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa mtaji wa mbuzi wa maziwa kupitia Mfuko wa maendeleo ya Jamii - TASAF III awamu ya II kwa ufadhili wa OPEC IV.
Wanawake hao, wameishukuru serikali wakati wakikabidhiwa mbuzi wa maziwa kwa ajili ya kufuga na kujiongezea kipato, zoezi lililofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya kijiji hicho.
Wamesema kuwa serikali imezijali kaya masikini, licha ya kuwapatia fedha za ruzuku lakini imeweza kuwapa mradi wa mbuzi wa maziwa, chakula cha kuanzia, mafunzo ya kitalamu pamoja na chanjo na kuahidi kuwatunza mbuzi hao vizuri ili waweze kuzaa na kuleta mafanikio kwenye familia zao.
Sara Lobulu (88) ameweka hisia zake kwa kumshukuru mama Samia kwa kuwakumbuka wanawake wazee na wajane, mradi ambao amekiri utakwenda kuwasaidia wanakaya hao kukuza kipato na kuweza kutunza familia.
"Tunaishukuru serikali, tunamshukuru mama Samia, ametusaidia sisi wanawake wenzake, ametambua namna tunaelemewa katika kutunza familia zetu, ameona ni vizuri kutusaidia kupunguza makali ya maisha". Amesema mama Sara
Elinita Rogathe mama wa watoto 4, naye licha ya kuishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuweziwezesha kaya masikini kupata mtaji wa mbuzi wa maziwa, mradi ambao wanaamini utazinufaisha kaya zao na kuziinua kiuchumi na kuahidi kutunza vizuri mbuzi hao ili waweze kuzaliana na kuongezeka.
Naye Diwani wa kata ya Ikiding'a Mhe. Francis Lukumai amemshukuru Mhe. Rais, Samia Suluhu kwa kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kujikwamua kutoka kwenye lindi la umaskini na kuwataka wanakaya hao kutumi fursa hiyo vizuri ili kukuza pato la kaya.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amewasihi wanavikundi hao kutunza mbuzi hao ili wawawezeshe kujikwamua kiuchumi, na kuongeza kuwa Serikali inatambua hali duni za wananchi wake na kuja na mkakati wa kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kupifia miradi ya TASAF.
"Leo tumekabidhi mbuzi 80 tunategemea tukirudi kukagua mradi tutakukuta wamezaliana mara mbili, hakikisheni mtaji huu unakua na kujikwamua kiuchumi, tusiwauze wala kuwachinja, mbuzi hawa ni wa maziwa nendeni mkahakikishe baada ya muda kila mwanakaya anakuwa na idadi kubwa ya mbuzi ili kufikia malengo ya serikali". Amesema Mkurugenzi Msumi
Awali Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Arusha, Grace Makema, amebainisha kuwa mradi huo uliibuliwa na walengwa hao, na kufanikiwa kukabidhiwa jumla ya mbuzi 80 wenye thamani ya shilingi milioni 22.1 wamekabidhiwa kwa vikundi vitano vyenye wanakikundi 15 sawa na kaya 75 zikinufaika kwa kila kikundi kupata mbuzi wa maziwa 16.
Ametaja kiasi hicho cha fedha kimejumuisha gharama za ununuzi wa mbuzi, mafunzo kwa wanavikundi, chakula cha kuanzia ufugaji, dawa kinga pamoja na ufuatiliaji kwa watalamau wa mifigo, na kuongeza kuwa , wanakaya hao watafuga mbuzi hao wa maziwa chini ya uangalizi wa serikali ya kijiji kupitia Afisa Ugani wa kijiji kwa kuwapatia mbinu bora za ufugaji pamoja na chakula cha kuanzia ufugaji.
Ikumbukwe kuwa, mradi wa TASAF ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na serikali ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi wa kupambana na umaskini nchini.
ARUSHA DC Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.