Na Elinipa Lupembe
Wanawake wanaonufaika wa mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, mradi unaotekelezwa na TASAF kijiji cha Nduruma, wamemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na serikalia yake kwa kuwajali kutokana na uwezo wao mdogo wa kumudu gharama za maisha huku wakithibitisha fedha hizo kuwasaidia kuhudumia familia zao hususani kipindi cha ukame mkali kilichopita mwaka huu.
Fatuma Omari, amemshukuru mama Samia na kuweka wazi kuwa fedha hizo zimewawezesha kina mama wengi kuwa wajasiriamali kwa kuanzisha biashara mbalimbali kupitia vikundi vyao vya kuweka na kukopa, vikundi ambavyo vinawawezesha kupata mitaji.
Naye Aisha Mollel licha ya kumshukuru mama Samia amesema kuwa fedha hizo za ruzuku zimesaidia familia nyingi kujikimu na mahitaji ya familia zao hususani chakula katika kipindi cha ukame uliotokea maeneo mengi na kusababisha kukosa chakula
"Wengi wetu hapa tunategemea kilimo ili kupata chakula mwaka uliopita hakukuwa na mvua, tumepita kipindi cha ukame, lakini kupitia fedha za TASAF familia hazijayumba tuliweza kununua chakula na mahitaji mengine ya familia". Amefafanua Aisha
"Tunamshukuru mama Samia, tunamuombea kwa Mungu, kwa kutupa fedha hizi, sisi kina mama hasa na familia zetu hatudhaliliki tena, watalaka, waliotelekezwa wajane wote wanamudu kuhudumia familia zao sasa, mimi nafuga kuku na nina mradi wa kupika vitafunwa ninauzia wanafunzi shuleni" Ameweka wazi Fatuma
"Kwa sasa hata kina mama wenye uwezo mdogo wa kifedha, tunajiamini na kujiona ni bora mbele ya jamii, kina mama tunajivunia kuwa na Rais mama mwenzetu, ametupa joto na ari ya kufanyakazi zaidi, kwa kujiona kila kitu kinawezekana bila kujali jinsi, kwa sasa kina mama tunapambana kutafuta riziki za familia zetu bila woga" Amesisitiza Julitha Mollel
Naye Mratibu wa TASAF halmashauri ya Arusha, Grace Makema, amesema kuwa zoezi la utoaji ruzuku kwa Kaya zilizo kwenye mpango wa Kunusu Kaya Masikini limefanyika na jumla ya kaya 11,159 kutoka vijiji 87 halmashauri ya Arusha, zimepokea fedha za ruzuku, huku jumla ya shilingi milioni 877.9 zikitolewa ikiwa ni malipo ya madirisha mawili la 13 na 14 ya mwezi Machi - Aprili na Mei - Juni 2023
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.