• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANUFAIKA TASAF ARUSHA DC WAFUNDWA.

Posted on: May 18th, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Halmashauri ya Arusha inatekeleza mkakati wa kutoa elimu ya Ustawi wa Jamii kwa wanufaika wa mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanufaika hao wa matumizi ya ruzuku ya fedha wanazopokea ili kufikia malengo ya serikali.

Mratibu wa TASAF Halmasahuri ya Arusha, Grace Makema, amesema kuwa, kila zoezi la ugawaji fedha linapofanyika, watalamu huhakikisha wanatoa elimu kwa walengwa juu ya mambo muhimu ya kijamii, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa namna bora ya matumizi ya fedha hizo, pamoja na kuwapa uelewa juu ya malengo ya serikali kutoa ruzuku hiyo kwa kaya zenye uhitaji.

Aidha amefafanua kuwa, serikali inatoa fedha hizo zikiwa na masharti ya kuzingatia, hivyo walengwa wa TASAF wanatakiwa kufahamu masharti ya fedha za ruzuku wanazopokea, pamoja na kuyatekeleza kwa usahihi, ikiwemo ruzuku ya msingi, ruzuku ya elimu na ruzuku ya afya kwa kaya hizo.

"Tunalazimika kutoa elimu, kutokana na uzoefu wa walengwa wanaopokea fedha kushindwa kutekeleza masharti na ruzuku na kusababisha kupoteza sifa, kama Halmashauri, tumejipanga kuwakumbusha kuzingatia masharti ya ruzuku ya fedha hizo, ikiwemo kuhakikisha watoto wanaosoma wanahudhuria masomo, watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kuhudhuria kliniki, na zaidi kuhakikisha ruzuku ya msingi inatumika kupata mahitaji muhimu na kuendelza pato la familia" ameweka wazi Mratibu Garace.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii, kata ya Mwandeti, Paulina Masoka, amekutwa na Kamera yetu akitoa elimu kwa Walengwa wa kijiji cha Losinoni kati, kata ya Oldonyowas, na kuweka wazi kuwa, ni kawaida kabla ya walengwa kupokea pesa, kupewa elimu ya masuala mbalimbali ya kijamii, yaliyopo na yanayoendelea kila siku.

"Hapa tunakumbushana, juu ya kuzingatia masharti ya ruzuku ya fedha wanazopoke pamoja na matumizi sahihi ya fedha hizo, zaidi tunawahamasisha kuunda vikundi vya kuweka na kukopa, lakini pia tumekumbushana juu ya malezi bora ya familia kwenye masuala ya Lishe bora na unyonyeshaji kwa watoto kwa siku 100, watoto kuhudhuria shuleni, kuwapeleka watoto kliniki, kujitokeza kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi mwezi Augost 2022, pamoja na kuwapeleka watoto kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio." ameweka wazi Paulina.

Hata hivyo wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini, kijiji cha Losinoni kati, wamewapongeza wataalam kwa kuwapa elimu itakayowafanya kutambua msingi wa ruzuku ya fedha wanazopokea pamoja na malengo ya serikali ya kuzikwamua kaya hizo kutoka kwenye hali ya uamsikini.

Mwenyekiti wa kijiji cha Losinoni kati, mheshimiwa, Peter Gabriel, licha ya kuishukuru serikali kwa kutoa ruzuku kwa kaya zenye uhitaji, ameipongeza Halmashauri kwa kutoa elimu kwa walengwa wa TASAF, kutokana na ukweli kuwa elimu hiyo itawawezesha kujikwamua kijamii na kiuchumi, hali itakayosababisha kuondokana na wimbi la umasikini uliokuwa unazikabili kaya hizo.

Mnufaika wa TASAF, Amani Ngeresa amewashukuru na kuwpaongeza watalamu, kwa kuwapa elimu inayowezesha kutambua namna ya kuzingatia masharti ya ruzuku, matumizi sahihi ya fedha hizo, elimu iliyowawezesha kufahamu lengo la serikali la kuondoa umasikini kwenye kaya zao.

"Tunashukuru kwa elimu tuliyopewa, awali hatukufahamu kuwa pesa hizo zina masharti yake, na hatukufahamu lengo la Serikali kwa undani, lakini sasa tumejua serikali inataka nini kwetu, na tunaahidi kutumia pesa hizi, kuunda vikundi vya kuweka na kukopa ili kupata mitaji ya kuanzisha biashara ndogogo ambazo tunaamini zitatuondoa kwenye umaskini uliokuwepo." Amesisitiza mnufaika Amani.

Awali halmashauri ya Arusha, ni miongoni mwa halmashauri zinazonufaika na mradi wa Mpango wa Kunusuru kaya masikini, unaotekelezwa na TASAF III, huku jumla ya kaya 13, 859 katika vijiji vyote 88 vya halmashauri ya Arusha zikinufaika.

"SENSA YA WATU NA MAKAZI AGOUST 2022

"JITOKEZE KUHESABIWA"✍✍✍







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.