Na Elinipa Lupembe
Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini halmashauri ya Arusha wametakiwa kuitunza, kuithamini na kuitumia vema miradi ya TASAF ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali.
Rai hiyo imetolewa na wajumbe wa Kamati ya kusimamia ofisi ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakikishi Zanzibar, walipotembelea miradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi Zahanati ya Likamba, mradi unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kata ya Musa.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Machano Othman Said, amesema kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa maendeleo na maslahi ya jamii nzima kwa kupambana na maadui watatu, ujinga, umasikini na maradhi.
Lengo la serikali kupitia mpango wa uhawilishaji fedha ni kuhakikisha kila kaya inapata mahitaji yake ya msingi huku miradi ya miundombinu ikiwezesha upatikanaji wa huduma za kijamii ndani ya maeneo wanayoishi.
"Tumeshuhudia miradi ilivyopendeza, wenyewe mmethibitisha umuhimu wa miradi hii kwenu, ni jukumu lenu sasa kuitunza ili idumu vizazi na vizazi lakini zaidi tumieni fursa hii kuibua miradi mingine zaidi" . Amesisitiza Mwenyekiti huyo
Akisoma taarifa ya mradi huo, Afisa Mtendaji wa kijiji, amesema kuwa mradi wa nyumba ya watumishi wa Afya yenye sehemu mbili (2in 1), umegharimu kiasi cha shilingi milioni 77 fedha kutoka serikalini kupitia TASAF IV OPEC III, unategemewa kuishi familia mbili za wahudumu wa afya wa zahanati hiyo ya Likamba.
Hata hivyo wanufaika wa mpango wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kijiji cha Musa, wameshukuru TASAF na kutoa shuhuda za namna mpango huo ulivyoleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii ndani ya kijiji chao.
"Tunaishukuru TASAF kwa kutufumbua macho, wanawake tulikuwa gizani, TASAF imetupa mafunzo ya kukabiliana na umasikini, leo tumeweza kukaa kwenye vikundi kuwekeza pesa na kukopeshana, tumeweza kushirikiana na kuanzisha miradi ya kuongeza kipato kwenye kaya zetu, tunaamini TASAF imeletwa na Mungu". Amesema Mary Lemburis
Sanare Sayuni amemshukuru Mhe. Rais Samia, kwa kuwajali wananchi wa hali ya chini, uwepo wa nyumba ya mtumishi kwenye zahanati hiyo, utaondoa vifo visivyo vya lazima vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua pamoja na uhakika wa upatikanaji wa huduma za afya kwa saa 24.
Wajumbe hao kutoka baraza la Wawakilishi Zanzibar wamefanya ziara ya mafunzo kwa siku tatu mkoani Arusha na kutembelea miradi 4 halmashauri ya Arusha na Meru.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#kaziinaendelea✍✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.