Na Mwandishi wetu
Washiriki wa michezo ya UMITASHUMTA halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuongeza juhudi katika mazoezi ili kuweza kukabiliana na mashindano ya michezo hiyo kimkoa na hata kitaifa ili kuweza kupata ushindi.
Akizungumza wakati wa kikele cha Masindano ya UMITASHUMTA, Mkuu wa Idara Elimu Msingi Halmashauri ya Arusha, Mwl. Salvatory Alute, katika kuchangua timu itakayoiwakilisha kimkoa na hatimaye Taifa, michezo iliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Ilboru.
Afisa Elimu Alute ameweka wazi kuwa wachezaji wote waliochaguliwa kuwakilisha Halmashauri ngazi ya mkoa, wanapaswa kujituma kwa viwango vya juu ili kuweza kuchaguliwa kushiriki mashindano hayo ngazi ya Taifa, kwa kuwa nafasi hiyo ni fursa ya kuibua vipaji na hatimaye kuwasaidia wachezaji kutimiza ndoto zao.
“Inafahamika michezo ni Afya, Elimu na Ajira hivyo niwasihi kujituma kwa kadri ya uwezo wenu, ili muweze kufikia malengo ya UMITASHUMTA na hatimaye kutimiza ndoto zenu, msikubali kukata tamaa kutokana na changamoto yoyote mtakayokutana nayo, na sisi kama viongozi tutajitahidi kutatua changamoto zinazowakumba ikiwemo vifaa vya michezo ili kuwawezesha wengi wenu kutimiza ndoto zenu”. Amesisitiza Mwl. Alute.
Hata hivyo, kaimu Afisa michezo halmashauri ya Arusha, Priscus Silayo, amesema kuwa lengo la kuandaa mashindano hayo ni kupata wanafunzi watakaoshiriki mashindano katika ngazi ya mkoai lakini pia kutwaa ubingwa wa michezo ya UMITASHUMTA kitaifa, licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakumba kama vile viwanja pamoja na vifaa vingine vya michezo.
Nao washiriki wa michezo hiyo wameeleza shauku yao katika mashindano hayo ni ushindi licha ya kuwa eanategemea michezo kuwa ajira hapo baadaye inayoweza kubalisha maisha yao, familia zao na Taifa kwa ujumla.
Jesca Lenard, Mwanafunzi wa shule ya msingi Trust Saint Patrick Schools, na mshindi wa mbio za mita 100 na mita 200 ngazi ya kitaifa msimu uliopita ameeleza matamanio yake na faida anayoipata katika michezo hiyo.
“Natamani kuwa mshindi mashindano ya riadha Taifa, ili niweze kufanikiwa katika maisha yangu na kuisaidia familia yangu kupitia kipaji changu, ninajifunza kuwa mvumilivu na kujituma zaidi kwasababu" Amesema Jesca
Awali, mashindano hayo ambayo yalianzia ngazi ya shule, kata, vitalu na wilaya,yakiambatana na kaulimbiu isemayo “Takwimu sahihi ni msingi wa mipango bora ya Taifa, shiriki sensa ya watu na makazi kwa maendeleo yetu”, yanajumuisha michezo ya mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, fani za ndani na ngoma pamoja na riadha, huku wanafunzi 250 wakishiriki pamoja na walimu 30 kutoka katika vitalu vitano, ambapo washiriki 120 wamechaguliwa kuiwakilisha Halmashauri ya Arusha katika ngazi ya Mkoa na hatimaye kitaifa.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
JIANDAE KUHESABIWA
PICHA ZA MATUKIO
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.