• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WASIMAMIZI WA MIRADI ARUSHA DC WATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI KWA WELEDI

Posted on: June 28th, 2021

Na.Elinipa Lupembe.

Wasimamizi wa miradi halmashauri ya Arusha, miradi inayotekelezwa na fedha za miradi kutoka serikali Kuu, kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2020/2021, wametakiwa kusimamia miradi hiyo kwa weledi na kuhakikisha, inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora unaoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Mipango, halmashauri ya Arusha, Anna Urio, wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kufuatilia hali ya utekelezaji wa miradi hiyo, katika sekta ya Afya na Elimu, miradi inayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.9.

Afisa Mipango huyo, amefafanua kuwa, licha ya kuwa miradi hiyo, inaendelea vizuri lakini amewasistiza, wasimamizi wa miradi hiyo, kuhakikisha wanafuata kanuni, sheria na taratibu za matumiz ya fedha za serikali huku wakihakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ubora na kwa wakati uliopangwa.

Aidha ameweka wazi kuwa miradi hiyo, inatelelezwa kwa kutumia 'forced account' na kusimamiwa na wakuu wa shule, wasimamizi wa vituo vya Afya pamoja na kamati za ujenzi katika maeneo hayo, na kuongeza kuwa kamati hizo zinatakiwa kufuata kanuni na taratibu zote zilizoainishwa kisheria huku wakihakikisha miradi hiyo inakuwa na uwiano wa majengo na thamani ya pesa walizopokea 'value for. money'

"Kwa wastani kasi ya ujenzi inakwenda vizuri, na miradi imekamilika kwa zaidi ya asilimia 50, hivyo niwatake wasimamizi wa miradi, kukabiliana na chngamoto za kimazigira zinazojitokeza pamoja na kuwahimiza  wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi, kwa kuwepo site kila siku, ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kuanza kuwahudumia wananchi" amesisistiza Afisa Mipango huyo.

Hata hivyo wajumbe wa kamati za ujenzi, ambao ni wasimamizi wa miradi hiyo, wamekiri kuendelea kujitolea kusimamia miradi hiyo kwa weledi, hasa kwa kutambua umuhimu wa serikali kuruhusu ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na  serikali yao.

Awali timu hiyo ilitembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa jengo la mionzi 'Xray', jengo la mama na mtoto 'RCH' Kituo cha afya Nduruma, ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi, ujenzi wa mabweni 6, ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na vyoo katika shule za sekondari na msingi.

ARUSHA DC

Kazi inaendeleea✍✍✍

PICHA ZA MIRADI

Timu ya ufuatilija utekelezaji wa miradi ya maendeleo, halmashauri ya Arusha, wakizungumza na wajumbe wa Kamati ya ujenzi ya miradi ya miwili ya jengo la mama na mtoto pamoja na ujenzi wa jengo la mionzi 'Xray' kituo cha afya Nduruma.


Mhandisi wa ujenzi halamshauri ya Arusha, Eng. Seleman Kiba akikagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Ilkiding'a

Mradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto kituo cha afya Nduruma



Timu ya ufuatilija utekelezaji wa miradi ya maendeleo halamshauri ya Arusha, ikikagua mradi wa ujenzi wa jengo la mionzi 'Xray' kituo cha afya Nduruma


Vyumba vya madarasa shule ya sekondari Ilkiding'a


Bweni la wavulana shule ya sekondari Einoti

Bweni la wasichana shule ya sekondari Einoti

Vyumba vya madarasa shule ya msingi Kambi ya Maziwa

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.