Na Elinipa Lupembe
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Angellah Kairuki amewataka wataalamu kusimamia utekelezaji wa miradi ya kuboresha na kuimarisha elimu ya Awali na Msingi (BOOST) kwa kufuata Miongozo, Sheria na Kanuni na taratibu zilizoainishwa.
Mhe. Waziri, ametoa wito huo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watalamu wa fani mtambuka kutoka ngazi ya Halmshauri na mikoa ya kanda ya Kaskazini, mafunzo yaliyofanyika kwenye shule ya Sekondari Ilboru wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha.
Mhe. Kairuki amewataka watalamu kutumia ujuzi na maarifa watakayoyapata kupitia mafunzi hayo kwenda kusimamia utekelezaji wa mradi wa BOOST katika maeneo yao ili kufikia malengo ya serikali ya mpango wa shule salama, zitakazomuwezsha mwanafunzi kuwa mahizi bila vikwazo.
"Kila halmashauri hakikisheni mnaelewa na kufuata afua zote za utekelezaji wa mradi kwa kuzingatia kanuni na taratibu, utunzaji wa nyaraka na uandaaji wa taarifa za mradi, tukamilishe miradi bila kuwa na hoja za ukaguzi" Amesisitiza Mhe. Waziri.
Aidha Waziri Kairuki, amebainisha lengo la serikali kupitia mradi wa BOOST ni kuwa na mpango salama wa shule, wenye mazingira rafiki yenye kupunguza vikwazo vya upatikanaji wa elimu kwa watoto pamoja na kuwajengea wanafunzi umahiri katika nyanja mbalimbali.
Hata hivyo Mhe. Waziri amewaonya wasimamizi wa utekelezaji wa mradi wa BOOST kuwa makini kwa kuepuka udanganyifu na ubadhilifu wa fedha hizo na kuweka wazi kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaokwenda kinyume na taratibu zilizoelekezwa na serikali.
Naye Naibu Katibu Mkuu OR - TAMISEMI, Ramadhani Kairima amesema kwa kanda ya Kaskazini jumla ya wanafunzi wakufunzi 274 watajengewa uwezo wa mradi huo kutoka mikoa ya Arusha, Manyara na Singida na kusisitiza kuwa utekelezaji wa miradi ya BOOST kuwa agenda ya kudumu katika vikao vya kisheria vya halmashauri zote.
Aidha ameeleza lengo la mafunzo hayo ni kuzijengea uwezo timu za utekelezaji wa mradi wa BOOST ili kuwa na uelewa wa pamoja, na kuwawezesha kufahamu vema mradi wa BOOST, malengo ya mradi, hatua za utekelezaji na namna bora ya utekelezaji unaozingatia kanuni, aheria na taraibu kwa kuzingatia matokeo chanya yanayotarajiwa na serikalia.
Mradi BOOST umezinduliwa rasmi katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini na unategemea kutekelezwa ka kipindi cha miaka mitano kuanzi mwaka wa fedha 2022/2023 - 2025/2026, unaotegemea kujenga jumla ya madarasa 12,000 kwa gharama ya shilingi trilioni 1.15 sambamba na kuimarisha matumizi ya TEHAMA shuleni, lengo kuu likiwa ni kuboresha elimu ya awali na msingi.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA UFUNZGUZI WA MAFUNZO
Waziri wa Nchi OR - TAMISEMI, Mhe. Angela Kairuki akifungua mafunzo ya wajumbe wa timu ya utekelezaji wa Mradi wa BOOST ngazi ya halmashauri na Mkoa, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano shule ya sekondari Ilboru wilaya ya Aruemru mkoani Arusha.
Naibu Katibu Mkuu OR - TAMISEMI, Ramadhani Kairima, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wajumbe wa timu ya utekelezaji wa Mradi wa BOOST ngazi ya halmashauri na Mkoa, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano shule ya sekondari Ilboru wilaya ya Aruemru mkoani Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wajumbe wa timu ya utekelezaji wa Mradi wa BOOST ngazi ya halmashauri na Mkoa, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano shule ya sekondari Ilboru wilaya ya Aruemru mkoani Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.