Na Elinipa Lupembe
Maafisa Watendaji wa kata 27 za halmashauri ya Arusha, wamesaini mkataba wa upangaji, ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli za Lishe kwenye maeneo ya kata zao, huku wakitakiwa kufanya kazi hiyo kwa kuzingatia malengo makuu mawili, viashiria na vigezo tisa vilivyoainishwa kwenye makataba huo.
Maafisa hao wamesaini mkataba huo baina yao na Mkurugezni Mtendaji halmashauri ya Arusha, Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Mganga mkuu pamoja na Mratibu wa Lishe, ikiwa ni hatua ya muendelezo wa uingiaji wa mikataba ya usimamizi wa shughuli za afua za lishe kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa, wilaya na na hatimaye ngazi ya kata na vijiji.
Akizungumza wakati wa zoezi la utiaji saini mikataba hiyo, Kaimu Mkurugenzi Halmashauti ya Arusha, Elizabeth Ngobei ameweka wazi kuwa, mkataba huo una malengo makuu mawili ikiwa ni kufanikisha suala la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo na kuhakikisha jamii inashiriki ipasavyo kupanga, kutekeleza na kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mpango wa halmashauri wa afua za lishe.
Amesema kuwa kwa kuzingatia malengo hayo Maafisa Watendaji ambao ni wasimamizi wapaswa kufanya kazi hiyo kwa weledi kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa, kulingana na vigezo na viashiria 9 vilivyoanishwa kwenye mikataba .
"Kila mtu anafahamu umuhimu wa afya bora katika maisha ya binadamu na ujenzi wa Taifa, Serikali imewapa jukumu hili muhimu, nendeni mkalitekeleze kwa umakini mkubwa kulingana na makubaliano, kama kuna changamoto tushirikishane kwa wakati ili kwa pamoja tufikie malengo yaliyokusudiwa na serikali". Amesisitiza Kaimu Mkurugenzi huyo.
Naye Mratibu wa Lishe, halmashauri ya Arusha, Doto Milembe, amefafanua kuwa, Mkataba wa lishe unawataka Maafisa Watendaji wa Kata kuhakikisha wanashirikiana na Maafisa Watendaji vijiji, kufanya kazi hiyo pamoja na kufanya tathmini na kutoa ripoti ya utekelezaji kwa kila mwezi.
"Lishe duni inanikusababisha umasikini katika Taifa kwani hakutakuwa na Jamii inayoweza kujituma kwa kufanya kazi kutoakana na watu wengi kuathiriwa na utapiamlo, viongozi wenzangu tupambane kutokomeza utapiamlo katika maeneo yetu,,ili kuwa na watu wenye afya bora"Amesisitiza Mratibu huyo wa Lishe.
Nao Maafisa Watendaji wa kata, wameahidi kwenda kufanyia kazi maelekezo yote kama yalivyo malengo yake kwa kuzingatia vigezo na viashiria vilivyoainishwa kwenye mkata, ikiwa ni pamoja na kuifanya agenda ya kudumu kwenye vikao vyote vya kisheria.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Bwawani Simon Kaaya amebainisha kuwa, wao kama watendaji wanalo jukumu kubwa la kuutekeleza mpango huo kwa vitendo kwa kuwa unawahusu wananchi moja kwa moja ambao wako chini ya mamlaka zao za vijiji na vitongoji.
"Mpango wa lishe ni muhimu kwa kuwa tunakwenda kuandaa wananchi wenye afya bora ambayo ni nguvu kazi ya taifa, tutatumia majukwaa yote kutoa elimu kwa makundi kwa kushirikiana na wahudumu wa afya ngazi ya jimii na kuhakikisha unakuwa na matokeo chanya" Amesisitiza Kaaya.
Ifahamike kuwa mkataba wa Lishe ni mkakati wa Kitaifa ambao ulisainiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma na baaye kusainiwa na wakurugenzi wa hamashauri kupitia ofisi ya Mkuu wa mkoa na hatimaye, kusainiwa na halmashauri ya Arusha.
Arusha DC
KaziInaendleeo ✍✍
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KUSAINI MKATABA WA LISHE
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.