Na Elinipa Lupembe.
Watoto wa kiume shule za msingi, wamebainisha kuwa chanzo kikubwa cha ulawiti kwa watoto wa kiume ni wazazi kushindwa kuwasimamia watoto wao katika malezi kwa kujikita zaidi kwenye kwenye mambo yao na kuwaacha watoto wakijilea wenyewe.
Watoto hao wametoa maoni hayo wakati wa midahalo ya kutoa elimu ya Ulawiti, iliyofanyika baina ya Kamati ya Kupinga Ukatili wa Ulawiti kwa wavulana 'Father on Duty' na klabu za Maabara za wavulana shuleni (Boy's Vac Lab), mdahalo uliofanyika kwenye shule 4 za msingi halmashauri ya Arusha.
Watoto wameelekeza malalamiko yao kwa wazazi kwa kueleza kuwa baadhi ya wazazi wamepoteza maadili kwa kufanya mambo mabaya mbele ya watoto na wengine kujikita zaidi kwenye kutafuta pesa za kuendesha maisha na kuwaacha watoto wakijilea wenyewe majumbani.
Hansa Masawe mwanafunzi (VI) shule ya msingi Ilboru, amebainisha kuwa baadhi ya wazazi na watu wazima hufanya vitendo vya ngono huku watoto wakiona jambo ambalo linawafanya watoto nao kuiga na kuanza kufanyiana wenyewe kwa wenyewe.
Lomnyaki Mollel mwanafunzi (5) shule ya msingi Olturoto amebainisha kuwa kwa sasa wazazi wanatumia muda mwingi kutafuta pesa za kuendeshea maisha na kuwacha watoto chini ya uangalizi wa ndugu, jamaa na marafiki, watu hao huanza kuwalawiti watoto na watoto huzoea na kuanza kufanyiana wenyewe kwa wenyewe.
Nasiri Shaban mwanafunzi wa shule ya msingi Naurei, ameeleza kuwa, tabia ya wazazi kuacha watoto wanalala na wageni wajapo nyumbani nayo ni chanzo cha ulawiti kwa watoto wa kiume, na kuwataka wazazi kuwacha tabia ya kuwalaza wageni kwenye vyumba vya watoto.
Hata hivyo wanavulana hao wamelalamikia, kitendo cha jamii kuwatetea watoto wa kike na kuwaacha watoto wa kiume kando, kimesababisha wakatili kugeukia kwa watoto wa kiume, madhara yake yameanza kuonekana, hivyo jamii inapaswa kuelekeza nguvu pia kupambana na ukatili dhidi ya watoto wa kiume hususani kwenye vitendo vya ulawiti.
Mratibu wa Kuthibiti Maambuki ya UKIMWI Halmashauri ya Arusha, Dkt. Japhet Champanda, ameeleza madhara ya watoto kulawitiwa kiafya ni pamoja na kushindwa kuzuia haja kubwa, kupata mamabukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo ya kiiingia sehemu ya haja kubwa ni vigumu sana kutibika.
"Athari za ulawiti, humuondrlea mwanaume urijali na kuathirika kisaokolojia kwa kushindwa kujiamini na kushindwa kutekeleza majukumu yake kama mwanaume" .Amesisitiza Dkt. Champanda.
Hata hivyo wajumbe wa kamati ya Father on Duty amewataka wamewataka watoto kukataa kuingiliwa na wanaume wenzanzao na kutoa taarifa pale wanapohisi mtu mwenye nia ovu ya kuwafanyia vitendo hivyo, pamoja kutoa taarifa za siri kwa walimu kama kuna watoto wanafanyiana vitendo hivyo.
Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na shirika la CWCD, linatekeleza mradi wa kupinga ukatili wa kingono na ulawiti kwa watoto wa kiume, kupitia maabara za wavulana 'Boy's Vac Lab' katika shule za msingi za Naurei, Moivo, Ilboru, Olturoto, Kiranyi na Ngaramtono kwa ufathili wa Foundation for Civil Society.
ARUSHA DC
KaziIendelee✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.