• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WATUMISHI MAKAO MAKUU ARUSHA DC, WAUNGA MKONO KWA VITENDO AGIZO DC ARUMERU LA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA YA OFISI KILA ALHAMISI

Posted on: February 3rd, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Watumishi wa makao makuu halmashauri ya Arusha (ARUDHA DC HQ) wameridhishwa na kupongeza agizo la mkuu wao wa wilaya ya Arumeru, la  kupanga siku ya Alhamisi kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka ofisi zao, jambo ambalo licha ya kuweka mazingira safi lakini pia linaongeza ushirikiano baina ya watumishi na kuleta hamasa katika utekelezaji wa kazi za kiutumishi.

Wakizungumza wakati wa kufanya usafi asubuhi ya leo, watumishi hao wameweka wazi kuwa, zoezi hilo la kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka ofisi zao ni la muhimu sana kwao, hasa kwa kuzingatia wahudumu waliopo ni wachache hawana uwezo wa kumudu kufanya usafi na kufikia maeneo yote kwa wakati, hivyo zoezi hilo limewezesha mazingira yetu kuwa safi.

Afisa Utumishi halmashauri ya Arusha, Elizabeth Ngobei, amesema kuwa, watumishi wameridhishwa na kujitoa kwa suala la kufanya usafi wa mazingira ya ofisi zao, kwa kuwa, licha ya mazingira kuwa safi lakini pia linakutanisha watumishi pamoja na kuongeza umoja baina yao huku likiongeza ufanisi katika kazi.

Naye Afisa Afya halmashauri ya Arusha, Issa Msumari, amethibitisha umuhimu wa watumishi kufanya usafi wa mazingira yao, unajenga umiliki wa maeneo yao, unaleta hamasa kwa wananchi kujituma kufanya usafi, na zaidi linaongeza tija na ufanisi katika kazi.

"Kufanya usafi wa eneo unapofanyia shughuli yoyote ni jukumu la kila mtu anayehusika na eneo hilo, hivyo hata sisi watumishi ni jukumu letu kufanya usafi katika maeneo yetu, hii inahamasisha hata wananchi wetu kuiga mfano kwa kufanya usafi kwenye ameneo yanayowazunguka" amethibitisha Afisa Afya Msumari.Aidha watumishi hao, wameshauri kuwa ili zoezi la usafi liwe la ufanisi zaidi, ni vema uongozi kuwaandalia  vifaa vya kutosha vya kufanyia usafi, ili kufikia lengo lililokusudiwa.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi, amewapongeza watumishi wote kwa mapokeo chanya ya kufanya usafi wa mazingira na kuahidi   uwepo wa vifaa vya kutosha wakati wa zoezi hilo."Ninawapongeza watumishi wote kwa kufanya usafi wa  mazingira, katika maeneo yote yanayozunguka ofisi za makao makuu ya halmashauti yetu, zoezi hili ni endlelevu na niwaahidi uwepo wa vifaa kila wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo" amesema Msumi.

Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, aliagiza watumishi wote wa halmashauri za wilaya hiyo Meru na Arusha, kufanya usafi ni zoezi endelevu kila siku ya Alhamisi lengo likiwa ni utekelezaji wa agizo la mheshimiwa Makamu wa Rais la kufanya usafi wa mazingira na kuhakikisha maeneo yote kuwa safi.


ARUSJA DC

KaziIendelee

PICHA ZA MATUKIO WATUMISHI WAKIFANYA USAFI




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.