Na Elinipa Lupembe
Watumishi sekta ya Afya wamekumbushwa kutekeleza majuku yao ya kazi, huku wakizingatia kanuni na taratibu za utumishi wa Umma, ili kufikia lengo la serikali la kiwahudumia wananchi.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu, halmashauri ya Arusha, Elizabeth Ngobei alipokutana na watumishi wa hospitali ya Selian Ngaramtoni, kwenye kikao kazi cha kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi hususani katika masuala ya haki na wajibu wa mtumishi wa Umma katika eneo lake la kazi.
Mkuu huyo wa Idara ya Utumishi, amewataka watumishi hao, kutambua kuwa, katika utumishi wao wa Umma, wanapaswa kutambua wanayodhamana kubwa ambayo Serikali imewaamini hivyo wana wajibu wa kutekeleza majukumu yao ya kitabibu ili kufikia lengo la serikali la kuwahudumia wananchi katika sekta hiyo ya Afya.
Elizabeth amewasisitiza kuwa, kila mtumishi anapaswa kutambua haki na wajibu wake unaozingatia maadili ya taaluma yake kazini na si vinginevyo na kuongeza kuwa serikali inapotoa haki ya kuajiri na kulipa mshahara mtumishi, mtumishi pia anaowajibu wa kutekeleza majukumu yake kutokana na haki hiyo anayopewa na serikali.
"Licha ya kazi ngumu mnayoifanya watumishi wa sekta hii ya afya, Serikali inatambua na kuthamini kazi yenu, hivyo ni vema kila mtumishi kufanya kazi kuendana a kasi ya maendeleo na kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea" Amesisitiza Afisa Utumishi huyo
Hata hivyo Elizabeth amewashauri watumishi hao, kujiendeleza kielimu kupitia taaluma walizoajiriwa nazo, ili kuongeza ufanisi katika kazi unaoendana na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia pamoja na kupanda madaraja na ngazi za mshahara.
Nao watumishi wa hospitali ya Serilan wameipongeza uongozi wa halmashauri hiyo, kupitia Idara ya Utumishi kwa kukutana na watumishi hao na kufanya kikao ambacho kimewapa uelewa na ufahamu mkubwa kwenye masuala ya utumishi wa Umma, pamoja na kuwajengea uelewa wa pamoja juu ya haki na wajibu wa watumishi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Asaria Giliad Mhudumu wa Afya hospital ya Selian, ameweka wazi kuwa, kikao hicho kimekuwa na matokeo chanya kwao, kwa kuwa wamepata fursa ya kuwa na uelewa wa pamoja kati ya mwajiri na mtumishi, sambamba wajibu wa mtumishi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kazi.
"Tumepata fursa ya kukumbushana mambo mbalimbali ya kiutumishi, ikiwemo masuala ya miundo ya utumishi, upandaji wa madaraja, michango ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na mafao ya kustaafu, mambo ambayo watumishi wengi yalikuwa yanatuchanganya" Amebainisha Elias Molle dreva wa Hospitali hiyo
Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Seliani Dkt. Amon Marti, licha ya kupongeza uwepo wa kikao kazi hicho, amewataka watumishi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ikiongozwa na nidhamu inayoongozwa na uzalendo ili kufikia malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi.
Awali Hospitali ya Selian ni miongoni mwa hospitali za halmashauri ya Arusha, inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini, ikiwa na jumla ya watumishi 111 wanaolipwa mishahara na serikali kupitia ruzuku, kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wanachi.
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
JIANDAE KUHESABIWA✍✍✍
Mkui wa Idara ya Utumishi, halmashauri ya Arusha Elizabeth Ngobei, akizungumza na watumishi wa hospitali ya Selian Ngaramtoni wakati wa kikao kazi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa kanisa la hospitali hiyo
Watumishi wa hospitali ya Selian Ngaramtoni wakifuatilia mada zilizotolewa wakatii wa kikao kazi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa kanisa la hospitali hiyo
Mhudumu wa afya hospitali ya Selian Ngaramtoni, Isaria Giliard akiuliza swali juu ya haki za mtumishi katika mafao ya kustaafu, wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa kanisa ndani ya hospitali hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa hospitali ya Selian Ngaramtoni wakifuatilia mada zilizotolewa wakatii wa kikao kazi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa kanisa la hospitali hiyo
Baadhi ya Watumishi wa hospitali ya Selian Ngaramtoni wakifuatilia mada zilizotolewa wakatii wa kikao kazi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa kanisa la hospitali hiyo
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.