WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUWAANDIKISHA WATOTO WALIOFIKISHA UMRI WA DARASA LA AWALI NA DARASA LA KWANZA 2025.
Kaimu Afisa Elimu Msingi Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bi. Scholastica Bura, amewataka Wazazi na Walezi kuhakikisha wanawaandikisha watoto wao waliofikia umri wa kuanza Darasa la awali na Darasa la kwanza Kwa mwaka wa masomo 2025.
Amesema kuwa Idara ya Elimu Msingi imejipanga vyema kuhakikisha malengo ya kufikisha asilimia 100 ya uandikishaji yanafikiwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu.
Aidha, Bi. Scholastica amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora.
Amebainisha kuwa Maandalizi ya ufunguzi wa shule yanaanza kwa kufanya vikao na Makundi muhimu, yakiwemo Waalimu wakuu na waratibu Elimu kata, ili kuweka Mikakati Madhubuti ya kusimamia Maendeleo ya elimu.
Kuhusu suala la chakula shuleni, Bi. Scholastica amesema kuwa ufaulu wa wanafunzi unahusiana moja kwa moja na upatikanaji wa chakula mashuleni.
Ameeleza kuwa mwaka 2024, asilimia 71 ya wanafunzi walipata chakula shuleni, lakini lengo la Halmashauri Kwa mwaka 2025 ni kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi wote wanapata chakula ili kuimarisha afya na utulivu darasani.
Bi. Scholastica pia amewataka Maafisa Elimu Kata kusimamia shule zao kwa karibu, kwa kushirikiana na watendaji wa kata na Wenyeviti wa vijiji, ili kuhakikisha wazazi wanatambua umuhimu wa kuwaandikisha watoto wao shuleni na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya elimu. @arusha_district_council @rc_mkoa_arusha
https://www.instagram.com/p/DEXJakbo9Kj/?igsh=aWl4cG8wYjF1MG05
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.