Na. Elinipa Lupembe.
Serikali kupitia wizara ya mambo ya Ndani ya nchi, imewahakikishia wananchi katika halmashauri ya Arusha, ulinzi na usalama kwa asilimia miamoja, kwa kuwa hilo ni jukumu la serikali yao.
Wananchi hao, wathibishiwa Usalama huo na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi, Mhe. Kange Lugola, wakati akiwahutubia wananchi wa halmashauri hiyo, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kituo cha mabasi Ngaramtoni na kuahidi kuanzisha wilaya ya kipolisi Ngaramtoni kutokana na ukuaji wa mji na ongezeko la idadi ya watu.
Akiwahutubia wananchi hao, pamoja kupokea kero na changamoto za wananchi, Waziri Lugola amesema kuwa, jukumu kubwa la serikali ni kuwapa haki na kuwahakikishia usalama wananchi wao bila kuwaonea wala kubagua.
Aidha amesema kuwa, serikali inatambua kuwa kuna baadhi ya watumishi wa jeshinla polisi ambao si waaminifu, bado hawatendi haki stahiki kwa wananchi, na kufanya hivyo ndio wanalichafua jeshi hilo na kuongeza kuwa serikali inaendelea na opereshi ya kuwaondoa.
Amewataka askari kufanya kazi zao kwa uaminifu kwa kufuata misingi na maafili ya kazi, ikiweomo kuacha kuwabughudhi wananchi hasa wakiwa katika maeneo yao ya kazi huku wakiendelea na shughuli zao halali.
Kangi Amepiga marufuku ukamataji wa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda na kufungia pikipiki zao polisi bila sababu za msingi hasa kwa makosa madogo madogo ambayo yanasababisha kero na bughudha kwa wananchi na familia zao.
Ameyataja makundi ya makosa yanayopaswa kukamatwa na polisi ni bodaboda zilizojihusisha na uhalifu wa aina yoyote, bodaboda zilizosababisha ajali pamoja na bidaboda isiyokuwa na mwenyewe.
Hata hivyo amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kulinda amani na usalama wao kwa kutii sheria bila shurti, kuacha tabia ya kuvunja sheria pamoja na kuacha tabia ya kutoa rushwa wajati wa kupata dhamana kwa watu waliokamatwa kwakuwa dhamana ni haki ya mtuhumiwa.
Katika mkutano huo, Waziribhuyo wa mambo ya Ndani nchini, ametoa gari kwa kituo cha Polisi Ngaramtoni na kumkabidhi mkuu wa kituo cha Polisi Ngaramtoni Bariki Kileo, na kuongeza kuwa gari hilo litumike kuwahudumia wananchi na kuhakikisha usalsma wa wananchi upatikana kwa asilimia mia moja.
Awali akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Arumeru, mbunge wa vuti Maalum Taifa, Mhe. Amina Mollel ameeleza kuwa kumekuwepo na askari wasiokuwa waaminifu wanaowanyanyanyasa vijana waendesha bodaboda kwa kuwakamata wao kinyume na sheriq pamoja na kufungia pikipiki zao, ilihali vijana hao wanazitegemea pikipiki hizo kwa ajili ya uzalishaji na kuendeshea maisha yao.
Katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya Ya Arumeru Mheshimiwa Jeri Cornel Muri alimuhakikishia Waziri huyo na wananchi wa Wilaya kwa ujumla kuwa wilaya hiyo imejipanga kukabiliana na changamoto zote za wananchi pamoja kuthibiti viashiria vyote vya Uhalifu
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya pia ameeleza kuwa tayari wilaya hiyo imefanikiwa kuwapata wadau wa Maendeleo watakaosaidia kuyakarabati magari yote mabovu ya Jeshi la Polisi katika wilaya hiyo ili iweza kulisaidia Jeshi la polisi kuimarisha Doria wilayani humo
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.