Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, mhe. Kassim Majaliwa, ametembelea kambi ya wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars) na kuwaeleza namna Serikali na wananchi wa Tanzania wana matumaini makubwa kwa timu yao, hivyo wahakikishe wanapata ushindi katika mechi yao dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda.
Waziri Mkuu huyo, ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Uganda, amewataka wachezaji hao wasiwe na wasiwasi kwa sababu hawana tofauti yoyote na wachezaji wa timu nyingine duniani.
“Macho yote ya Watanzania yameelekezwa katika mechi ya kesho na Serikali ina matumaini makubwa na timu ya Taifa, hivyo waelewe kwamba kesho ni siku muhimu sana. Lengo letu ni kufikia hatua ambayo mataifa mengine yamefikia”.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kamati yake itatoa shilingi milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu hiyo iwapo timu itafuzu kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika #AFCON2019
Makonda amesema Watanzania wanachokijua kwa sasa ni kwamba AFCON 2019 ni zamu yao, hivyo wanawaomba wachezaji wa timu ya Taifa wahakikishe wanawapa furaha, kwa kuifunga timu ya Taifa ya Uganda na kwamba wananchi wengi wamehamasika kwenda kuwashangilia.
Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala ameahidi kuwapeleka katika mbuga ya wanyama kwa ajili ya mapumziko iwapo wachezaji hao wataibuka na ushindi katika mechi yao dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda hapo kesho.
Awali, Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samata amesema,”Ninafuraha si kwa sababu ya ukubwa wa mechi ya kesho bali ni kwa sababu naona kesho nakwenda kuongoza nchi. Tupo tayari kuliletea Taifa ushindi”.
SHIME WATANZANIA TUIUNGE MKONO TIMU YETU YA TAIFA*
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.