• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI MKUU: VIONGOZI WETU WANAMATUMAINI NA MICHEZO YA FEASSSA

Posted on: September 18th, 2022

Na Elinipa Lupembe

 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanamatumaini makubwa kuwa mashindano ya shule za msingi na Sekondari za Afrika Mashariki (FEASSSA) yataendelea kuwa chachu kwa nchi washirika kuendelea kuthamini michezo.

Amesema kuwa viongozi hao wanaamini kupitia michezo hiyo ya FEASSSA itaendelea kusaidia katika kukuza ajira, kustawisha jamii, uchumi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Amesema hayo leo (Jumapili, Septemba 18, 2022) wakati akizindua Mashindano ya michezo ya shule za msingi na za Sekondari kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa Mamlaka zote zinazosimamia elimu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea kuwajengea mazingira rafiki vijana wanaoshiriki michezo ya FEASSSA ili kutanua wigo wa ushindani ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

“Ni vyema sasa viongozi wa FEASSSA kushirikiana kwa karibu na vyama vya michezo katika nchi za Afrika Mashariki na vilabu vya michezo mbalimbali kutupia macho vipaji vinavyopatikana katika mashindano haya ya wanafunzi ili kupata wachezaji watakaokuwa na mwendelezo na kuvitumikia vilabu vyao.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka viongozi wa Mashirikisho ya Michezo ya shule katika kila nchi husika kuwa na mipango ya pamoja ya muda mfupi na muda mrefu ya maendeleo ya michezo ya shule. “Mipango hiyo itumike kuhamasisha utekelezaji wa mikakati ya kuendeleza michezo katika taasisi za elimu ndani ya Jumuiya.”

Amesema ni vyema pia viongozi wa chama hicho kutoa fursa kwa walimu wa michezo wa nchi wanachama kubadilishana uzoefu ili kuboresha ufundishaji wa michezo shuleni.

Mheshimiwa Majaliwa amesema michezo hii ya FEASSSA itasaidia kuwafanya wanafunzi kuwa na afya njema ya akili na mwili, hivyo kuboresha ufundishaji na kuendeleza vipaji vya wanamichezo mahiri.

“Ni wazi kuwa matatizo mengi ya kiafya kwa wanadamu yanaongezeka kutokana na mfumo mpya wa maisha tunayoishi ambao hautupi muda wa kushiriki shughuli za michezo. Watu wanaoshiriki katika michezo imewasaidia kupunguza matatizo mengi ikiwemo matatizo ya msongo wa mawazo, shinikizo la damu, kisukari na uzito uliopitiliza”.

Awali, akizungungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa David Silinde amesema, anamshukuru Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya dhati ya kuwezesha na kuendeleza michezo hususan katika shule za msingi na sekondari.

“Lengo la FEASSSA ni kuimarisha umoja, mshikamano na kuwajengea vijana wetu uzalendo.”

Naye, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Michezo vya Shule za Sekondari Afrika Mashariki (FEASSSA) Justus Mugisha Amesema moja ya malengo ya Michezo hiyo ni kuhakikisha wanazalisha vijana wataoweza kushiriki katika michezo mbalimbali ili kuzitangaza nchi za Afrika Mashariki.

“Tunajua vijana hawa hapo baadae watakuwa sehemu ya timu zetu za Taifa na hatimaye kuitangaza jumuiya yetu, hii ndio maana tunaamini katika michuano ya mashule Ikiwemo hii ya FEASSSA.”

 

SOURCE :IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU.





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.