Na. Elinipa Lupembe.
Halmashauri kuanzisha mchakato wa kuipandisha hadhi halmashauri ya Arusha, kuwa halmashauri ya Mji na baadaye kuwa Manispaa, kwa kuwa tayari halmashauri hiyo ina sifa na vigezo stahiki. Hii ni kutoka na ukubwa wa eneo la halmashauri unaokwenda sambamab na ongezeko kubwa la idadi ya watu, wanahitaji kupata nyingi karibu na maeneo yao tofauti na ilivyo sasa.
Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, ifanye ziara ya kutembelea nyumba iliyoko eneo la Engira Road, inayomilikiwa na halmashauri mbili za Meru na Arusha, ili kuishauri Baraza alMadiwani namna bora ya matumizi ya mradi huo, ambao ni chanzo cha mapato na kinashindwa kufanya vizuri kutokana na umiliki wa pande mbili.
Mamlaka za serikali, zinazotoa huduma ndani ya halmashauri ya Arusha, ikiwemo Mamlaka ya Maji Mijini na Vijijini - RUWASA, Mamlaka ya Barabara Mijini na Vijijini - TARURA na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Arusha - AUWSA, zimetakiwa kupanga mtalamu atakayewajibika moja kwa moja kutekeleza majukumu ya huduma wanazotoa kwa kushirikaiana na Watalamu wa halmashauri, ili kuwa na malengo ya pamoja katika kutatua changamoto ya utekelezaji wa miradi ya maji na barabara, lengo likiwa ni kuwaondolea kero zinazotokana na kusuasua kwa huduma hizo kwa wananchi.
Halmashauri kuimarisha Kamati ya usimamizi wa uendeshaji Mitambo ya halmashauri kwa kuhakikisha mitambo hiyo inafanya kazi ya kukarabati miundombinu ya barabara katika maeneo ya halmashauri hiyo, kutokana na uharibifu mkubwa wa barabara uliotokana na mvua zilizonyesha mwaka uliopita, pamoja na kukodisha mitambo hiyo ili kupata fedha kwa ajili ya matengenezo ya mitambo hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wameupongeza uamuzi wa watalamu wa halamshauri ya Arusha, kwa kuanzisha shule mpya ya mchepuo wa kiingereza Enaboishu Academy, kama chanzo endelevu cha mapato, na kuwataka watalamu kuendelea kubuni vyanzo vingine vipya, huku wakiendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vilivyopo na kuthibiti mianya ya upotevu wa mapato, unaosababbishwa na baadhi ya watu wasio waaminifu.
Wheshimiwa Madiwani wamehimizwa kushirikiana na watalamu katika kusimamia vyanzo vya mapato vilivyopo katika maeneo yao, na kutambua kuwa wana jukumu la kuvisimami kwa kushirikiana na watalamu, kwa kuwa Mapato ya halmashauri ndio nguzo ya kuendesha halmashauri, na ndio injini ya kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Wananchi wametakiwa kuona umuhimu wa kurasimisha maeneo wanayomiliki na kutoa ushirikiano kwa watalamu wanahusika na zoezi hilo katika maeneo yao, hii ni kufuatia zoezi la urasimishaji ardhi na makazi linaloendelea katika maeneo mengi Halmashauri ya Arusha.
Aidha, Wajumbe wa Baraza la Madiwani wamewapongeza watalamu wa halamshauri ga Arusha kwa kujitoa kufanyakazi kwa bidii na kuifanya halamshauri hiyo, kung'ara kwa kufanya vizuri katika tathmini za halamshauri za mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mwenyekitinwa halmashauri ya Arusha, mheshimiwa Ojung'u Salekwa, akihutubia wajumbe wa Baraza la Madiwani, wakati wa kuhitimisha mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili mwaka wa fedh 2020/2021, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule akifafanua jambo, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili mwaka wa fedh 2020/2021, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyoendelea, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili mwaka wa fedh 2020/2021, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Afisa Mipango halmashauri ya Arusha, Anna Urio akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili mwaka wa fedh 2020/2021, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Diwani wa Kata ya Oloirieni, Mhe. Erick Semboja, akichangia hoja, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili mwaka wa fedh 2020/2021, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.