******RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI*
#Nimefurahishwa sana na hatua hii ya utiaji saini wa ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli zilizokuwepo, dhumuni ni kuboresha huduma ya usafiri katika Ziwa Victoria.
#Ukarabati wa meli 2 za Mv Butiama na Mv Victoria utagharimu Shilingi Bilioni 27.61, tumeamua kufanya ukarabati mkubwa.
#Meli ya Mv Liemba iliyopo mkoani Kigoma nayo tumepanga kuikarabati.
#Tunatekeleza miradi hii yote kwa manufaa ya watanzania wote, tumeamua na hatutarudi nyuma, watanzania tunaweza.
#Tusikwepe kodi ndugu zangu watanzania, kodi ni msingi wa maendeleo ya Tanzania.
**** MHANDISI ISACK KAMWELWE-WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO*
#Utekelezaji wa miradi hii ni juhudi zako Mhe. Rais Magufuli, za kuhakikisha unasimamia vyema makusanyo ya fedha za watanzania.
#Tunakushukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutoa fedha ambapo mpaka sasa tumeshakarabati meli tano.
#Maziwa tunayo tunapaswa kuyatumia kuhakikisha tunafikia uchumi wa kati.
*****SONG GEUM YONG- BALOZI WA KOREA KUSINI NCHINI*
#Nawapongeza wahusika wote kwa kusaini mkataba wa utekelezaji wa ujenzi wa meli mpya na chelezo.
#Maendeleo haya yote yanatokana na juhudi kubwa zinazofanywa na watanzania wakiongozwa na Rais Dkt. John Magufuli
#Tanzania na Korea Kusini ni wabia wazuri sana katika masuala ya maendeleo hasa baada ya Tanzania kufungua ubalozi nchini Korea.
****ERICK HAMISI- KAIMU MENEJA MKUU- KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI*
#Ujenzi wa meli hii ya kisasa katika Ziwa Victoria utagharimu shilingi bilioni 88.76 na itakuwa na uwezo wa kubeba tani 400 za mizigo, abiria 1200 na magari madogo 20.
#Meli hii itakuwa kubwa kuliko zote za Ukanda wa Maziwa Makuu, itakuwa na urefu wa mita 90 na kimo cha mita 10.9 sawa na ghorofa 3 kwenda juu.
#Ujenzi wa meli hii utakamilika katika kipindi cha miezi 24.
#Ujenzi wa meli hii mpya utaajiri watanzania si chini ya 250.
#Pia tutasaini mkataba wa ujenzi wa chelezo (slipway) itakayotumika kujenga meli mpya katika Ziwa Victoria, chelezo hii ikikamilika itakuwa na uwezo wa kubeba meli yenye uzito wa tani 4000.
#Chelezo hii itakuwa na urefu wa mita 100, ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 35.99 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12.
****MHE. SELEMANI KAKOSO(Mb)-MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MIUNDOMBINU*
#Tunaahidi kamati itakuwa pamoja nawe katika jitihada hizi za utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.
*Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO*
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.